Kocha
wa Kimataifa wa Mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
katikati akiwasimamia mazoezi mabondia Faraji Sayuni kushoto na Hassani
Kiwale wakati ya mazoezi yao yanayoendelea katika kambi ya Super D coach
Uhuru GYM Kariakoo Dar Es Salaam
Na Mwandishi Wetu
MPAMBANO wa ubingwa wa taifa wa kg 57
utagombaniwa na mabondia Kais Rashidi Na Faraji Sayuni siku ya Agost 8
katika ukumbi wa Kobelo Pub Manzese Dar Es Salaam
mpambano uho wa raundi kumi za ubingwa
umeratibiwa na Promot Miraji Uliza ambapo kutakuwa na mapambano mengine
mbalimbali ya mchezo wa masumbwi nchini
mabondia wengine watakaopanda siku
hiyo ni Abdallah Pazi atakaezipiga na Said Mkone wakati godrack Mrema
atakumbana na Hassani Kiwale wakati Omari Uliza atazipiga na Bruno
Fadhili na Said Jelemi atamkabili Azizi Kondo na Saleh Mkalekwa atacheza
na Salum Ngula na Azizi Uliza atacheza na Mohamed Matimbwa
pamoja na mapambano mengine mengi
Katika
Mchezo huo kutakua na Uuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi
pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na
kocha 'Super D'
kwa ajili ya kuwapa mabondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki
kujua sheria za masumbwi.
Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd
Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David
Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa
yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano
makubwa matano ya utangulizi
|
No comments:
Post a Comment