















Mkuu wa mkoa wa Kagera Mohamed Babu akikata utepe kuzinduwa mnara mpya wa Zantel wa huduma za intaneti jijini Bukoba. Pembeni kwake ni Mkuu wa kitengo cha mahusiano ya umma na matukio wa Zantel William Mpinga.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mohamed Babu akitumia huduma ya intaneti ya Zantel baada ya hafla fupi ya kuuwasha mnara mpya wa intaneti eneo la Kibeta, Bukoba. Pembeni yake ni Mkuu wa kitengo cha mahusiano na matukio wa Zantel William Mpinga.
Mkurugenzi wa Matawi na Utawala wa Shirika la Nyumba la Taifa Bw. Raymond Mndolwa akitangaza uamuzi wa shirika hilo kutoa muda wa hadi tarehe 28 mwezi huu kwa wadaiwa wa shirika hilo kulipa madeni yao, kinyume na hapo shirika hilo litachukua hatua ya kutoa vitu vyao vya ndani na kuvipiga mnada. Kushoto ni Mkuu wa Elimu kwa Umma na Huduma kwa Jamii Bi. Susan Omari.
Meneja Mwandamizi Huduma kwa Biashara ya Serikali(NMB) Bi. Domina Feruzi (katikati) akikabidhi msaada wa mabati kwa Afisa Elimu kata ya Sinza Bi. Phoibe Ileta kwa niaba ya shule za Msingi za Sinza na Sinza Mashujaa. Kushoto ni Mwenyekiti wa Shule ya Msingi Sinza Bw. Flavian Mgori.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Sinza wakitoa burudani ya ngoma.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB.
Wanafunzi wa Shule za Msingi za Sinza na Sinza Mashujaa zilizopokea msaada wa mabati hayo.