Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, February 4, 2011

BOT YATETEA NOTI ZA 'BATIKI'


BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa ufafanuzi kuhusu utowaji wa rangi katika noti mpya na kusema kuwa hali hiyo ni ya kawaida kwa noti zilizochapwa kwa teknolojia maaluum ijukanayo kama 'Intaglio Printing'

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu alisema aina hiyo ya uchapishaji unafanya noti kuwa na hali ya mparuzo zinapopapaswa na imetumika ili kuimarisha kingo za noti kwa lengo la kupunguza uwezekano wa kuchanika na kuchakaa kwa haraka.

Prof.Ndulu alisema miparuzo hiyo huacha rangi noti inaposuguliwa kwa nguvu kwenye karatasi nyeupe kitendo ambacho kinathibitisha kuwa noti hiyo ni halali.

"Kutoa rangi ni moja ya arama ya usalama inayothibitisha kuwa noti siyo bandia,noti hizi hazichuji zikilowekwa kwenye maji kama inavyodaiwa kwa kuwa wino uliotumika hauyayuki katika maji"alisema Prof.Ndulu

Prof.Ndulu alisema kuwa utowaji wa rangi huo upo hata katika noti za nje kama dola pale zinaposuguliwa ambapo teknolojia iliyotumika kutengezewewa inalingana.

Alisema kuwa noti hizo zimetengenezwa kwa teknolojia ya kuwekewa kinga dhidi ya uchafu ili kupunguza uwezekano kunasa uchafu inapokuwa katika mzunguko.

Aliongeza kuwa noti za zamani bado ni halali na zitaendelea kutumika pamoja na zile mpya mpaka zitakapopotea katika mzunguko kwa sababu ya uchakavu wake.

Akizungumzia kuwepo kwa noti mmoja iliyo na thamani kubwa zaidi ya sh.10,000/- alisema BoT haikuona haja ya kufanya hivyo kwakuwa malipo makubwa yanahimizwa kufanywa kupitia njia ya nyingine za kibenki kama njia ya mitandao.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...