Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, February 16, 2011

VIDEO YA SUPER D BOXING COACH KUTOKA MWEZI UJAO


BONDIA wa Zamani na Kocha wa Ngumi wa Klabu ya ngumi ya Ashanti, Rajabu Mhamila
'Super D' yupo mbioni kutoa Video inayozungumzia maisha yake ya mchezo huo.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Super D alisema video hiyo itakuwa sokoni muda
wowote kuanzia sasa ikizungumzia maisha yake tangu alipoanza kucheza mchezo huo
mwaka 1984 hadi 2010 sasa.
Alisema Video hiyo itaonesha mapambano mbalimbali aliyocheza na dhidi ya
mabondia Mbwana Matumla, Rashidi Ali na Ajibu Salumu.
Alisema lengo la kuandaa video ni kutaka kutimiza malengo yake ya kuendeleza
mchezo wa ngumi kwa kuwapatia vijana nafasi ya kujifunza kupitia kwake.
Alisema kutokana na nchi ya Tanzania kuwana vipaji vingi atashindwa kuwafikia
kila mmoja wao na badala yake amewapa fursa ya kujifunza kwa kuangalia video.
Alisema Video katika kuhaikisha Video hiyo inafanya vizuri sokoni ameongezea
vionjo vingine kutoka kwa mabondia maarufu duniani kama Mike Tyson, Michael Mo,
Junior Myweather, Mohamed Ally, Man Paqyao na Joe Fleizer.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...