Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, February 10, 2011

KAMPUNI YA BIA TBL YAKABIDHI MRADI WA MAJI SAFI NA SALAMA


Matenki ya Maji safi na Salama yaliyowekwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika shule ya msingi ya Daraja mbili,iliyopo Mkoani Arusha.Matenki haya wamewekwa katika shule hiyo ili kuifanya shule hiyo iweze kujipatia maji safi na salama kutokana na mradi unaoendelezwa na kampuni hiyo ya bia hapa nchini.Mradi huu wa maji safi na salama uliogharimu kiasi cha sh. mil. 17 utasaidia kupunguza,kuutokomeza kabisa uhaba wa maji safi na salama kwa shule hiyo pamoja na wakazi wa maeneo ya jirani na shule hiyo.
sehemu ya mabomba ya maji hayo ikiwa bado haijamalizika vizuri,huku mafundi wakiendelea na shughuli yao ya uboreshaji wa karo la kuhifadhia maji hayo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...