Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, February 18, 2011

HASHIMU LUNDENGA AKIJIFUA

Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga, akijikunja kupiga shuti kali, wakati wa mazoezi ya timu yake ya Rose Garden, yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Posta Kijitonyama leo asubuhi. Lundenga alijigamba kuwa mbali na kuandaa mashindano ya warembo na kutoa warembo bomba wanaokwendaa kushiriki katika mashindano ya Dunia kila mwaka, lakini bado hata katika Soka anaweza kufanya vizuri tena kuwazidi hata wachezaji wa Ligi Kuu kutokana na uzoefu wake wa siku nyingi katika mchezo huo kwa kutumia zaidi akili kuliko nguvu.
"Unajua mchezo wa soka ni akili zaidi na si miguvu japo kwa sasa mimi akili inakuwa inataka lakini mwili hautaki, lakini bado najiamini kuwa ninauwezo wa kufanya vizuri niwapo uwanjani tena hata kuwazidi baadhi ya wachezaji wetu ambao nimekuwa nikiwaona mara kadhaa wanarukaruka tu uwanjani" alisema Lundenga
Golikipa, Abdulrazak Jackson (kulia) akimkabili mshambuliaji, Hanrold Shangari, wakati wa mazoezi ya timu ya Rose Garden, yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Posta Kijitonyama leo asubuhi.
Kibwana Matokeo (kulia) akichuana kuwania mpira na Gerald Nyendela, wakati wa mazoezi hayo.


http://sufianimafoto.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...