Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, February 16, 2011

Iker Casillas bado alia na mwamuzi

MADRID,Hispania

MLINDA mlango wa timu ya Real Madrid, Iker Casillas amesema wazi kwamba hakustahili kutolewa nje ya mchezo kati ya timu yake dhidi ya Espanyol wa michuano ya Ligi Kuu ya Hispania uliofanyika Jumapili iliyopita jioni.

Mlinda mlango huyo wa timu ya Taifa alitolewa nje ya mchezo huo baada ya kuoneshwa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi mchezaji Jose Callejon nje eneo la penalti zikiwa ni dakika mbili tangu mchezo huo uanze na picha za video zinaonesha kuwa hakukuwepo na kosa kubwa la kustahili adhabu hiyo.

Casillas anaamini kwamba hakustahili kupewa kadi hiyo na anapingana vikali na uamauzi wa mwamuzi wa pambano hilo.


"Kadi yangu nyekundu inatia shaka lakini kama mwamuzi aliona ni sahihi basi tunapaswa kuikubali,"alisema mlinda mlango huyo kupitia tovuti ya klabu.

“Jambo la muhimu ni kwamba timu ilicheza soka safi na ilistahili kuwa kati ya wachezaji 10 kwa 10.Kiwango chetu kilikuwa juu na sisi tukafanikiwa kuondoka napointi tatu muhimu kwetu,”aliongeza.

Mbali na kulalamikia kadi hiyo,mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 29 alimpongeza mchezaji aliyingia kuchukua nafasi yake Antonio Adan akisema kuwa Adan alicheza mechi ngumu na atakuwa na mafanikio siku za mbeleni

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...