Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, February 24, 2011

BANK YA AZANIA YAZINDUA TAWI ARUSHA


Na Mwandishi wetu
BENKI ya Azania imeweza kutoa mikopo yenye thamani ya zaidi sh. bil 100/= kwa

wajasiriamali wadogo nchini hadi ilipofikia Desemba mwaka jana.

MkurugenzI Mtendaji wa Benki hiyo Charles Singili aliyasema hayo juzi katika
hafla ya ufunguzi wa tawi jipya la Mbauda la benki hiyo lililopo mkoani Arusha.

Singili alisema benki hiyo imekuwa na mafanikio makubwa kiutendaji na kwamba
mafanikio hayo yamewawezesha kufanikiwa kumudu changamoto za huduma za kibenki
nchini.

Alisema pamoja na huduma nyingine benki hiyo imekuwa mhimili mkubwa katika
kuinua uchumi wa Tanzania kwa kuhakikisha inaboresha hali za maisha ya
watanzania kwa kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa wajasiriamali katika nyanja


tofauti.
“Tunapaswa kujipongeza wenyewe lakini pia kuwapongeza wale wanaotuunga mkono
kwani tumekuwa na mafanikio makubwa yaliyotuwezesha kutoa mikopo ya thamani ya
zaidi ya sh. bil 100/= mpaka ilipofika mwishoni mwa mwaka jana,”alisema Singili.

Aliongeza kuwa pamoja na hilo wameweza kuimarika kwa kuongeza mtaji wa benki
ambapo ilipoanzishwa mwaka 2000 walikuwa na mtaji wa thamani ya sh. mil 700/=
lakini mpaka sasa wamefanikiwa kufikisha mtaji wa thamani ya sh. bil 18/=.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi wa benki hiyo William Erio alisema benki hiyo


imekuwa na mikakati endelevu kuhakikisha inaendelea kujiimarisha ambapo
aliwataka wadau wa benki hiyo kudumisha umoja wa kazi uliopo.

Alisema wataendelea kujitahidi kuhakikisha utendaji wa benki hiyo unakwenda
sanjari na mahitaji ya jamiii ya kitanzania katika kukabiliana na changamotio za


kiuchumi na kupunguza umasikini miongoni mwa watanznaia.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha Isidori Shirima aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla
hiyo akimwakilisha Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo aliipongeza benki hiyo kwa
mafanikio waliyofikia na kwamba wayachukue mafanikio hayo kama changamoto ya
kuendelea kujiimarisha.

Alisema serikali imekuwa ikiwategemea wadau tofauti wa maendeleo katika
kujikwamua kiuchumi na kwamba sekta ya kibenki ni miongoni mwa wadau hao hivyo
benki ya Azania haina budi kujizatiti katika kuhakikisha inaendelea kukua.

Mwisho. Mawazo Waziri
Media Relations Manager
Capital Plus International (CPI)
Phone: 022 2125431
Cell: +255 715 027 892
+255 754 027 892
+255 684 000 645

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...