Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, February 9, 2011

TOT PLAS KUIBUKIA VALENTINE DAY

Kundi zima la Tot Plus Taarab, siku ya Wapendanao 'Valentine Day', yaani tarehe 14/2/2011, litarindima katika ukumbi wa Traverine Hotel, Magomeni jijini Dar es Salaam, katika onyesho maalum la kuzindua albamu yake mpya ya 'TOP IN TOWN', kwa maelezo zaidi tafadhali soma bango lao hilo kwa makini.

WASANII WA TAARAB WAKIWA KAZOEZINI LEO


KIONGOZI wa kundi la TOT Plus Taarab, (wapili kulia) akiongoza baadhi ya wasanii wa kundi hilo kufanya mazoezi, leo katika ukumbi wa CCM, Mwinjuma, Dar es Salaam, jana. Mazoezi hayo ni kwa ajili ya uzinduzi wa albamu mpya ya kundi hilo ya 'Top in town' utakaofanyika Jumatatu, ijayo, katika ukumbi wa hoteli ya Travertine, Magomeni. Wengine kushoto ni Aziza Jumaa, Rukia Juma na Hemedi Omari.
Mwanamtama Amir na Sharifa Mohammed wakiwa kwenye mazoezi hayo
Kutoka kushoto, Mwasiti Suleiman, Omari Ali 'Kopa Jr', Mariam Khamis ak paka mapepe wakiwa katika mazoezi hayo
Rukia Juma, akifanya mazoezi
Tahabiti Abdul akicharaza kinanda kwenye mazoezi hayo
http://bashir-nkoromo.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...