Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, February 4, 2011

ALLY CHOKI AIBOMOA TWANGA PEPETA

KIongozi wa kundi la Extra Bongo Ally Choki akiwa na wasanii nane aliowapata kutoka Twanga Pepeta na kuwatambulisha mbele ya wana habari leo

5 comments:

 1. Siyo ajabu kwa wanamuziki kutoka bendi moja hadi nyiongine,na hii siyo mara ya kwanza kwa jambo hili kutokea katika historia ya muziki Tanzania.Yote ni kutafuta maisha na maendeleo puia hakuna wa kulaumiwaa hapa.Tunaona uongozi wa Twanga pepeta unalalamika sana wakati wao ndio wa kwanza kuvuruga bendi za wenzao,Mkuki kwa nguruwe.Hongerz Ally Choki,kaza buti tupo pamoja na wewe,na usikubali kutishwa na mtu yeyote.
  mdau Kinondoni,Dar.

  ReplyDelete
 2. NAMUUNGA MKONO MTOA MAONI WA FEB.13/KINONDONI,NI KWELI SIYO JAMBO LA AJABU KWA WANAMUZIKI KUTOKA BENDI HII NA KUHAMIA NYINGINE,HATA MIMI NASHANGAA HII ISHU IMEKUWA KUBWA UTAFIKIRI ALLY CHOKI KAUA MTU??WATU WAMEMSHUPALIA CHOKI BILA KUKUMBUKA KUWA HIYO TWANGA HUWA INAVUNJA BENDI NYINGI TU.UONGOZI WA TWANGA UKUMBUKE KUWA SIKU HIZI AU MIAKA HII NI YA USHINDANI NA SIYO YA WANAMUZIKI KUFUATA SIFA,WATU WANATAFUTA MASLAHI MAZURI NA SIYO KUTAJIRISHA WAMILIKI WA BENDI NA KUFANYISHWA KAZI KAMA PUNDA,MALIPO MADOGO NA MUDA WA KUPUMZIKA KWA WANAMUZIKI HAUPO KABISA.ANGALAIA SASA AKINA KALALA,CHOKORAA WANAENDELEA VIZURI NA BENDI YAO MPYA.WASANII/WANAMUZIKI HUU NI WAKATI WA KUAMKA
  KUWA WAANGALIFU NA MIKATABA YA KITAPELI,NA NINGESHAURI KABLA HAMJASAINI HIYO MIKATABA YENU HASA KWENYE BENDI KAMA TWANGA.TAFUTENI WANASHERIA WAIPITIE KWANZA NDIPO MSAINI,VINGINEVYO MTAAMBULIA SIFA,MIAKA INAPITA UMRI UNAONGEZEKA MNAISHIA KUWATAJIRISHA HAWA WAMILIKI WAROHO.HATA MIMI NASEMA ALLY CHOKI KAZA BUTI USITISHWE NA MTU YEYOTE,TANZANIA YETU NI NCHI HURU,HAKUNA BINADAMU NAYEMMILIKI BINADAMU MWENZIE. MIKA,LONDON,UK.

  ReplyDelete
 3. Ndugu mwana blog ya Burudani,nimeona afadhali nipitie ktk blog yako ili ujumbe wangu umfikie huyu dada Khadija Kalili wa Bongoweekend,hii ni kuhusu tatizzo la Twanga na Ally Choki,kwanza ningependa kumlaumu sana kwa kujipedekeza saana tena kwa wazi wazi kwa Twanga pepeta,habari yoyote mbaya au ya ukweli dhidi ya Twanga huwa haitoi,sasa sijui blog yake inamilikiwa na Twanga???maana Twanga wanaonekena wanapenda sana kumiliki binadamu wenzao !!!lakiani huu ndio mwisho wao,ushauri wa bure ni kuwa namuomba huyu dada awe mwana blog asiyependelea upande wowote la sivyo blog hii haitakuwa na maana na sisi tutakacha maana blog ni nyingi,tutakuwa hatusomi blog yake!!Dunia ya sasa ni ya utandawazi kuna njia nyingi za kupeleka ujumbe katika jamii na ukafika,hata kama utaukacha!!Kumbuka hata Misri serikali ilidiriki hata kufunga internet na mawasiliano mengine lakini wananchi waliweza kuwasiliana na kaafanikiwa kuitosa serikali dhalimu.Sioni maana ya kumuona Ally Choki kama adui wa nchi au muuaji,kuhama kwa wanamuziki ni jambo la kawaida,wanamuziki wanachoshwa na maisha duni na kutumiwa na hawa wanaojiita wamiliki wa bendi,kazi ngumu bila mapumziko malipo madogo,lazima watoke wakatafute maendeleo na maisha ya mafanikio yao na familia zao, na siyo misifa ya bure,nadhani mawazo yangu yanalingana na watoa maoni walionitangulia hapa.Dada Khadija acha kujipendekeza kwa Twanga(wazi wazi) ili Blog yako ipate maendeleo,huu ni ushauri wa bure nategemea ujumbe huu utafika kwa huyu dada,Blogs ni nyigi na sisi siyo wajinga tunazifuatilia kwa karibu saana dada jirekebishe.
  Charles,Dubai.

  ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...