Linah Sanga katika mwonekano wa picha tofauti.
Na Kambi Mbwana, Handeni
MWIMBAJI wa muziki wa
kizazi kipya hapa nchini, Linah Sanga, maarufu kama Lina, amesema huwa haogopi
kubambiwa na mashabiki wake, ndio maana amekuwa mwepesi kuwahitaji kila
anavyofanya shoo zake.
Linah aliyeibukia katika taasisi ya kukuza na kulea vipaji
ya Tanzania House of Talents (THT), ni miongoni mwa wasanii wanaofanya vyema mno katika tasnia ya
muziki wa kizazi kipya nchini.
Akizungumza na Handeni Kwetu, Linah alisema kwamba anapenda
kucheza na mashabiki wake kila anavyoona inafaa, hivyo anaamini aina hiyo
itaendelea kwa ajili ya kujipa amani na kuwapa fursa mashabiki wake kucheza nae
jukwaani.
Alisema katika maeneo mengi, hasa kwa kuangalia amani,
amekuwa akihitaji mmoja wao kwa ajili ya kuacha amani na heshima kwa mashabiki
wake, hivyo lengo lake haliwezi kusitishwa na woga wa kucheza, au kubambiwa na
mashabiki wake.
"Huwa napenda sana kucheza na shabiki wangu katika shoo
ninazofanya, hivyo siogopi kubambiwa, ingawa najua watu ukiwapa nafasi hiyo
wanakuja jukwaani na kucheza kwa fujo hasa wale wanaowakamia wasanii.
"Nafanya hivyo kwakuwa sina woga na ndio maana mashabiki
wangu nawaacha katika furaha kwa kushangilia, hivyo kwakweli hili ni lengo
langu zaidi, ili mradi tu kuwe na amani kwa kuimarishwa ulinzi, hasa katika
shoo kubwa.
No comments:
Post a Comment