Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga
(wa tatu kulia) akiwasili katika Kiwanda cha kutengeneza dawa za
binadamu cha Shelys kilichopo Mwenge jijini Dar huku akiwa ameambatana
na Mkurugenzi wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira (Enviromental Impact
Assessment-EIA) wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira
(NEMC) Bw.Ignace Mchallo ( wa pili kulia), Mkurugenzi wa Kurugenzi ya
kufanikisha udhibiti wa Mazingira Mhandisi Dr. Robert Ntakamulenga na
Wataalamu wa Kitengo cha Mazingira kutoka katika Wizara yake katika
muendeleo wa ziara za kushtukiza Viwandani kukagua mfumo wa mazingira ya
maji taka yenye kemikali katika viwanda hivyo kama unaendana na viwango
vilivyowekwa.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga
akieleza dhumuni la ziara yake katika kiwanda hicho kwa Afisa Rasilimali
watu wa Kiwanda cha dawa cha Shelys Bw. Nissa Mwaipiana (kulia).
Mkuu wa Idara ya Kuhakiki ubora wa Kiwanda hapo Bi. Shemina Pera Somji akitoa maelezo kwa Naibu Waziri na Ujumbe wake.
Mkuu wa Idara ya Kuhakiki ubora wa Kiwanda hapo Bi. Shemina Pera Somji
akimwongoza Mh. Charles Kitwanga kwenda kukagua sehemu ya kutibu maji
taka yenye kemikali.
Mwendesha Mashine wa Kiwanda hicho Bw. Patrick Mapunda (mwenye koti)
akitoa ufafanuzi Kwa Naibu Waziri Mh. Charles Kitwanga wa namna
wanavyokusanya na kuyatibu maji taka yanayotokana na uzalishaji kiwanda
hapo.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles
Kitwanga akitoa maagizo wa NEMC baada ya kutoridhishwa na mfumo wa maji
taka ya kiwanda hicho kutofikia ubora unaotakiwa.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles
Kitwanga(wa pili kulia) akiongozwa na Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha
soda cha CocaCola cha jijini Dar Bw. Ernie Van Vreden (kulia) kwenda
kukagua maeneo mbalimbali ya kiwanda hicho. Country PAC Manager wa
kiwanda hicho Bw. Evans Mlewa (wa pili kushoto) na kurugenzi wa
Tathmini ya Athari kwa Mazingira (Enviromental Impact Assessment-EIA) wa
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw.Ignace
Mchallo.
Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha soda cha CocaCola cha jijini Dar Bw.
Ernie Van Vreden akitoa Maelezo kwa Mh. Kitwanga juu ya Mitambo Mipya ya
Kisasa yenye kiwango cha Kimataifa kwa ajili ya kutibu maji taka katika
Kiwanda hicho.
Mh. Kitwanga na Ujumbe wake ukitizama Bwawa la Samaki linalotumika
kufanyia majaribio ya maji taka ambayo yamekwisha safishwa kwa ajili ya
matumizi mengine kiwandani hapo.
Mh. Charles Kitwanga (kulia) akitoa maoni yake baada ya ziara ya
kukagua maeneo mbalimbali ya kiwanda cha CocaCola na kuridhishwa na
utaratibu unaotumika katika uzalishaji wa bidhaa zao na mfumo wa
kuhifashi maji taka na kuyasafisha kwa njia ya kisasa na kuitaka kampuni
hiyo iwe mfano wa kuigwa na iwe Mwalimu kwa Makampuni mengine.
Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Soda cha CocaCola Bw. Basil Gadzios
(katikati) akitoa shukrani kwa Mh. Naibu Waziri na kuahidi kutoa
ushirikiano wa kitaalam kwa viwanda vingine juu ya utunzaji wa maji taka
na namna ya kuyasafisha kisasa kuepuka kuharibu Mazingira na kuongeza
kuwa Kampuni ina mkakati kabambe kwa mwaka 2013 kutengeneza ajira kwa
vijana ambapo inakusudia kujenga vituo katika maeneo mbalimbali kwa
ajili ya vijana kukusanya chupa za plastiki zinazotokana na kiwanda
hicho kwa ajili kuzalishwa upya.
Naibu Waziri Mh. Charles Kitwanga katika picha ya pamoja na Meneja Mkuu
wa Kiwanda cha CocaCola Bw. Basil Gadzios na Ujumbe wa NEMC na Maafisa
wa Wizara yake.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles
Kitwanga (wa pili kushoto) akiwasili katika Hotel ya White Sands jijini
Dar es Salaam kujionea jinsi Hoteli hiyo iliyopo ufukweni mwa bahari
inavyotunza mazingira yake. Kulia ni Meneja Mkuu wa Hoteli ya White
Sands Alwyn Kellerman na Afisa Mazingira wa Hoteli hiyo Bi. Linda Mbuya.
Mmoja wa wafanyakazi wa Hoteli hiyo akifunua chemba inayopitisha maji
taka kwa ajili ya kukaguliwa na jopo la wataalam kutoka NEMC na Maafisa
wa Wizara. Katika ukaguzi huo Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga hakuridhishwa na jinsi hoteli hiyo
inavyoendesha mfumo wake wa maji taka na kuagiza timu ya wataalam kutoka
NEMC kufanya ukaguzi upya wa mifumo hiyo.
Meneja Mkuu wa Hoteli ya Giraffe Ocean View Bw. Nicholas Oyieko akitoa
maelezo kwa Naibu Waziri Mh. Kitwanga (wa pili kushoto) jinsi hoteli
hiyo inavyotunza mazingira na namna inavyodhibit mfumo wake wa maji taka
kuhakikisha kwamba haileti madhara.
Hii ni sehemu iliyoko pembeni ya Hoteli ya Giraffe ambayo mmiliki wake
hafahamiki ambayo imewekwa uzio na kufanya bahari kushindwa kupumua
vizuri na kusababisha mkusanyiko wa uchafu unaodaiwa kutuama mahali hapo
tangu mafuriko ya hivi karibuni yaliyoikumba jiji la Dar es Salaam.
Naibu Waziri ameamuru muhusika kutafutwa mara moja na kupigwa faini na
kuamuriwa kuondoa vifusi hivyo.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga na ujumbe wake wakiangalia eneo hilo.
No comments:
Post a Comment