


Ramadhan Pazi akiingia katika gari lake aina ya Toyota Noah.


MSHINDI wa Bahati Nasibu ya 'Timiza
Ndoto Yako, Jishindie Toyota Noah' ambayo ilikuwa inaendeshwa na Kampuni
ya Global Publishers & General Enterprises Ltd, Ramadhan Salum
Pazi, mkazi wa Buguruni-Rozana jijini Dar es Salaam, leo amekabidhiwa
gari lake aina ya Toyota Noah. Makabidhiano hayo yamefanywa na Mbunge wa
Jimbo la Kinondoni, Idd Azzan nje ya ofisi za Global Publishers. Bahati
Nasibu hiyo iliyokuwa inaendeshwa kupitia magazeti ya Global ambayo ni
Uwazi, Risasi, Championi, Amani, Ijumaa na Ijumaa Wikienda ilifika
mwisho Desemba 20 mwaka jana ambapo bwana Ramadhani Pazi aliibuka
kidedea.
No comments:
Post a Comment