Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, January 11, 2013

SAMSUNG YACHEZESHA DRAW YA MSIMU WA SIKUKUU


 
Meneja Usambazaji wa Samsung Mobile Tanzania, Sylvester Manyara(katikati) akisoma zawadi ya mshinndi wa kwanza wa TV nchi 40 yenye thamani ya shilingi milioni mbili na nusu.Kushoto ni  Msimamizi wa Bahati na sibu Tanzania, Abdalah Hemed na Mkufunzi wa Samsung Tanzania, Joel Laizar Dar es Salaam.
Meneja Usambazaji wa Samsung Mobile Tanzania, Sylvester Manyara(kushoto),Msimamizi wa Bahati na sibu Tanzania, Abdalah Hemed na Mkufunzi wa Samsung Tanzania, Joel Laizar wakionyesha zawadi za washindi mara baada ya kuchezesha droo ya Samsung ya msimu wa sikuu ya X’mass na Mwaka mpya Dar es Salaam.Zawadi zote zinathamani ya shilingi milioni 6.
 
““Samsung LED TV 40”, Simu za Galaxy S3… Zapata washindi wake!” 
KAMPUNI ya SAMSUNG Tanzania leo imechezesha Draw kubwa kwa wateja wake walioshiriki ofa maalum ya msimu wa sikukuu. Ofa hiyo iliyojulikana kama “Samsung Season’s Offer!” ilianza rasmi mwishoni mwa mwezi wa kumi na moja mwaka jana na leo hii imefikia tamati. Draw hii imechezeshwa katika duka la Samsung lililoko Quality Centre, Dar Es Salaam. 
Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Mkuu wa Samsung Tanzania Bwana Kishor Kumar alisema, “Ofa hii ililenga kuwazawadia wateja wetu katika msimu wa sikukuu. Wateja wetu wengi walijishindia zawadi za papo kwa papo kama vile T-shirts za Samsung, Kofia, Kalamu nk. Tuko hapa leo hii kutimiza ahadi yetu, kuchezesha Draw hii kwa ajili ya kuwazawadia wateja wetu wenye bahati watakaonyakua zawadi hizi”. Draw hii ilisimamiwa na wawakilishi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha.
Naye meneja usambazaji wa Samsung Mobile Tanzania Bwana Sylvester Manyara alisema kwamba, “Pamoja na bidhaa nyingine za Samsung, bidhaa zilizokuwa katika ofa hii kabambe ni aina ya Galaxy Note 2, Samsung S3, Galaxy Note 10.1, Samsung S Duos, Samsung ACE Duos, Galaxy Pocket na Galaxy Pocket Duos.” Bwana Manyara aliendelea kuelezea kwamba wateja waliponunua bidhaa hizi katika msimu wa sikukuu walipewa kuponi maalum ambazo walijaza na kuzikusanya ili kujaribu bahati yao katika Draw hii. Ofa hii iliendeshwa katika maduka ya mawakala wa Samsung Dar, na katika maduka ya Samsung yaliyoko Mbeya, Arusha, Dodoma na Mwanza. 
Bwana Kishor Kumar alizitaja zawadi za Draw hii kwamba ni;
1.    Zawadi ya Kwanza; Samsung LED TV ya Inchi 40’.
2.    Zawadi ya Pili; Samsung Galaxy S3 Mobile Phone.
3.    Zawadi ya Tatu; Samsung Galaxy Note 10.1.
4.    Zawadi ya Nne; Samsung Home theatre.
5.    Zawadi ya tano; Samsung Smart Camera. 
Bwana Kishor alimaliza kwa kuwashukuru wateja wa Samsung kwa kuchagua bidhaa hizi bora, aliwaomba waendelee kufurahia bidhaa hizi hata baada ya msimu wa sikukuu. Aliwakumbusha kwamba miongoni mwa manufaa ya bidhaa za Samsung ni kwamba bidhaa zake ndio tu zina warantii ya miezi 24 yaani miaka miwili. Aliwakumbusha pia kupiga namba ya huduma kwa wateja endapo wakihitaji ufafanuzi wa jambo lolote kuhusu bidhaa za Samsung. Namba ya huduma kwa wateja wa Samsung ni +255 685 88 99 00. 
Mwezi wa kumi na moja mwaka jana, Samsung ilifanya maonyesho makubwa ya bidhaa zake jijini Dar Es Salaam, maonyesho hayo yaliyofahamika kama “Samsung Week” yalifanyika katika hoteli ya Golden Tulip. Samsung inafanya pia shughuli nyingi za kujitolea, hususani msaada wa udhamini wa mafunzo kuinua vipaji vya wanariadha katika shule ya Winning Spirit Arusha, msaada kwa shule na matibabu katika kijiji cha Ilmorijo Monduli Arusha na Lyamungu Moshi nk.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...