Bingwa wa kickboxing, Hamis Mwakinyo, anatarajia kupanda ulingoni kuzipiga
na bingwa wa Taifa wa ngumi za kulipwa nchini uzito wa light weight kg
60, Said mundi, wa Tanga katika pambano la raundi nane.
SAIDI MUNDI KUSHOTI NA KING CLASS MAWE |
Pambano
hilo litakuwa ni maalum kwa ajili ya kusindikiza pambano la ubingwa wa
mabara wa WBF kati ya Alan kamote na Jumanne Mohamed, litakalopigwa
katika uwanja wa mkwakwani jijini Tanga Machi 17, mwaka huu.
Hamis Mwakinyo ambaye ni bingwa wa ngumi na mateke afrika mashariki na kati wa WKN-AFRIKA
(World kickboxing Network- Afrika) na ameshawahi kuchalenji ubingwa wa
dunia nchini iran, atazichapa na mpinzani wake huyo, ambapo pambano hilo
linatarajiwa kuwa na upinzani mkubwa.
Aidha pambno hilo limezidi kuwa gumzo midomoni mwa mashabiki wengi wa mchezo huo, mkoani Tanga.
Kwa mujibu wa muandaaji wa pambano hilo Promota, Ally Mwanzoa, amesema kuwa mabondia hao tayari wameshakubaliana na kuridhia kutiliana saini mkataba wa makubaliano wa pambano hilo.
Mwanzoa, alisema kuwa pia kutakuwa na mapambano mengi ya utangulizi kwa mabondia kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania hususani jijini Dar es salaam na anategemea kuongeza nguvu za majaji wa mchezo huo kutoka nje ya Tanzania ili kuondoa malalamiko yeyote yanayoweza kujitokeza.
No comments:
Post a Comment