Mkuu wa Masoko wa Vodacom Tanzania Bw.Kelvin Twissa (kushoto) na
Meneja wa biashara wa kimataifa wa Fenix International, Peter Glenn
wakimshuhudia mkazi wa Kibaha Bi Anna Joseph,wakati akionesha kwa
vitendo jinsi chaja mpya aina ya Readyset inavyounganishwa kabla ya
matumizi,uzinduzi wa chaja hiyo inayotumia nishati ya jua,ina uwezo wa
kuchaji simu zaidi ya 10 kwa siku, matumizi ya redio, kuzalisha mwanga
wa hadi masaa 30. Uzinduzi na hatimaye kuanza rasmi kwa matumizi ya
kifaa hicho hususan kwa maeneo yaliyo nje ya gridi ya Taifa umefanyika
Dar es Salaam kupitia ubia baina ya Vodacom Tanzania na Kampuni ya Fenix
International.
Mkazi wa Pangani, Wilaya ya Kibaha, Pwani, Anna Joseph,
akionesha waandishi wa habari jinsi ya kutumia aina mpya ya chaja
inayotumia nishati ya jua 'ReadySet' iliyozinduliwa Dar es Salaam kwa
ushirikiano wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom na Fenix
International. Mkazi huyo amewaeleza waandishi wa habari kuwa amekuwa
akijipatia kipato cha hadi sh elfu 80 kwa mwezi kupitia kifaa hicho kwa
kuchajisha simu za wateja wake.
Mkuu wa Masoko wa Vodacom Tanzania Bw.Kelvin Twissa (kushoto)na
mkazi wa Kibaha Bi Anna Joseph ambaye ni mmoja wa wadau walionufaika na
huduma ya chaja za Readyset,wakiwaonesha waandishi wa habari (hawapo
pichani) namna chaja hizo mpya na zinatumia nishati ya jua zinavyofanya
kazi . Uzinduzi na hatimaye kuanza rasmi kwa matumizi ya kifaa hicho
hususan kwa maeneo yaliyo nje ya gridi ya Taifa umefanyika Dar es Salaam
kupitia ubia baina ya Vodacom Tanzania na Kampuni ya Fenix
International. Wanaoshuhudia nyuma ni Meneja wa biashara wa kimataifa
wa Fenix International, Peter Glenn, na Mkurugenzi Mtendaji wa Fenix
International,nchini, Peter Mungoma.
Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Vodacom, Kelvin Twissa,
akisisitizia umuhimu wa kila mtanzania hususan wajasiriamali waishio
maeneo yasiyo na umeme kutumia aina mpya ya chaja inayotumia nishati ya
jua maarufu Readyset ambayo pamoja na mambo mengine ina uwezo wa
kuchaji simu zaidi ya 10 kwa siku, matumizi ya redio, kuzalisha mwanga
wa hadi masaa 30. Uzinduzi na hatimaye kuanza rasmi kwa matumizi ya
kifaa hicho hususan kwa maeneo yaliyo nje ya gridi ya Taifa umefanyika
Dar es Salaam kupitia ubia baina ya Kampuni ya simu za mikononi ya
Vodacom na Kampuni ya Fenix International
Mkurugenzi Mtendaji wa Fenix International, Peter Mungoma
akionyesha kupitia 'projector' aina mpya ya chaja inayotumia nishati ya
jua, maarufu kama 'ReadySet Charger' ambayo pamoja na mambo mengine ina
uwezo wa kuchaji simu zaidi ya 10 kwa siku, matumizi ya redio,
kuzalisha mwanga wa hadi masaa 30. Uzinduzi na hatimaye kuanza rasmi kwa
matumizi ya kifaa hicho hususan kwa maeneo yaliyo nje ya gridi ya Taifa
umefanyika Dar es Salaam kupitia ubia baina ya Kampuni ya simu za
mikononi ya Vodacom na Kampuni ya Fenix International
---
Dar es Salaam, Aprili 5, 2013 -
Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom
imezindua chaja mpya za simu 'Readysety' zinazotumia nishati ya jua na
zenye uwezo wa kuchaji zaidi ya simu 5 tofauti kwa wakati mmoja kwa
minajiri ya kuwawezesha watanzania hususan waishio maeneo yasiyo na
umeme kupata mawasiliano ya uhakika kupitia simu zao za mikononi.
Readysety hizo pamoja na mambo mengine zinatumika kuzalisha mwanga kwa balbu ya aina yoyote kwa matumizi ya nyumbani na mahala pa biashara, na zaidi zina viunganishi kwa matumizi ya umeme wa kawaida.
Kukamilika na hatimaye uzinduzi wa chaja ya ReadySety ni matokeo ya ushirikiano wa kibiashara baina ya Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom nchini na Fenix International baada ya kujiridhisha juu ya ubora na faida zake kwa watanzania hususan wajasiriamali waishio maeneo yaliyo nje ya gridi ya taifa.
Akizungumza katika uzinduzi huo, kwenye duka la Vodacom, MlimaniCity, Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom nchini, Rene Meza, alisema ReadSety zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza fursa za mawasiliano na uhitaji zaidi wa simu za mikononi kwa watanzania waishio maeneo yote mjini na vijijini
"Watanzania waishio nje ya gridi ya taifa, ambao mara kadhaa hupata adha ya kusafiri umbali mrefu pale wanapohitaji fursa za nishati ya umeme kwenye kuchaji simu zao sasa wamepata jawabu," alisema Meza na kuongeza:
"Zaidi ya watu bilioni 1.3 duniani wanaishi bila huduma ya umeme na kuna watumiaji wa simu za mikononi takribani milioni 600 wanaoishi bila kutumia umeme wa gridi kitu ambacho kinawalazimu kutumia karibu dola za Kimarekani bilioni 10 kila mwaka kwa ajili ya kuchaji simu kwa kutumia jenereta na betri za magari," alisema Meza
Aliongeza kuwa Kampuni ya Vodafone na Vodacom ina watumiaji wa simu zaidi ya milioni 100 duniani kote ambao hawajaunganishwa na gridi ya
No comments:
Post a Comment