Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, June 1, 2013

Big Brother Africa: Washiriki watano waingia danger zone, wawili kutoka Jumapili hii
Baada ya saa 24 kupita toka mchezo uanze big brother alitoa tangazo la washiriki watano walioingia katika hatari ya kuiaga Big Brother “The Chase” Jumapili hii (June 2).

Majina ya washiriki walio katika hatari ya kutoka ni matano lakini watakaofungasha mizigo yao Jumapili hii ni wawili kati yao.

Upande wa Rubies House walio katika list hiyo ni hawa:


Selly wa Ghana

Natasha kutoka Malawi.
Upande wa Diamond House panga la eviction limemdondokea Betty wa Ethiopia baada ya mkuu wa nyumba hiyo Fezza kumuokoa mshiriki wa Ghana Elikem ambaye ndio aliyekuwa amechaguliwa na Big Brother.

Betty wa Ethiopia
Moja ya mamlaka aliyonayo mkuu wa nyumba ni pamoja na kumuokoa mshiriki anayekuwa amechaguliwa kutoka, kwa kumpendekeza mshiriki mwingine kwa niaba yake.

Washiriki wengine waliongia katika hatari ya kutoka weekend hii ni muwakilishi wa Kenya Huddah Manroe, pamoja na Denzel kutoka Uganda.


Huddah Manroe

Denzel

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...