Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, June 1, 2013

NIKI MBISHI, CHID BENZI WAMUENZI NGWEA


Na Elizabeth John


MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Chid Benz ameachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘R I P Ngwea’ akiwa na lengo la kumkumbuka msanii wa muziki wa hip hop, Albert Mangwea aliyefariki Mei 28 mwaka huu, nchini Afrika Kusini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Chid Benz alisema mashairi ya ngoma hiyo, yanazungumzia mazuri yote aliyokuwa anayafanya Ngwea enzi za uhai wake hadi anapofikwa na mauti.

“Ngwea alikua ni mtu ambaye anaelewa kitu anachokifanya katika muziki wake na najua hakuna shabiki ambaye alikua anazichukia kazi zake klutokana na uwezo wake wa kusimama katika mashairi,” alisema Chid.

Katika hatua nyingine, mkali wa muziki huo, Niki Mbishi ameachia kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Imeandikwa’ ambayo pia ni ya kumuenzi msanii huyo.

Niki Mbishi alisema wimbo huo tayari umeanza kusikika katika vituo mbalimbali vya redio na kwamba anawaomba mashabiki wa muziki huo wampe sapoti katika kumuenzi nyota huyo.

“Kiukweli Ngwea ni kati ya wasanii ambao walikua wanakubalika katika jamii, binafsi namuombea apumzike kwa amani, yeye katungulia sisi tutafuata,” alisema Niki MbisI.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...