Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, June 1, 2013

BALOZI PETER KALLAGHE APOKEA ZIARA YA KOMBE LITAKALOSHINDANIWA KATIKA AFRICAN NATIONS CUP UK KUANZIA LEO
 Balozi kallaghe (kushoto) akipokea Kombe kutoka kwa Timu ya Waandaaji wa masjindano ya Kombe la African Nations Cup UK , yatakayoshirikisha Timu 20 za Nchi za jamii ya kiafrika zinazoishi Uingereza (African Dispora). Mashindano hayo yameanza kutimua vumbi hii leo jijini London.
  Ballozi Kallaghe akikabidhiwa Kombe na Waandalizi ikiwa kama ishara ya Timu za Zanzibar Islands na Tanzania kushiriki katika mashindano hayo. Pichani wa kwanza kushoto ni  Kocha / Kiongozi wa Timu ya Tanzania Abdul Kassim, akifuatiwa na kijana Dula , Kapteni wa Tanzania Team. Pembeni ya Balozi ni Director wa Tanzania Trade Centre Mr Yusuph Kashangwa.
 Balozi Kallaghe akimkabidhu Captain wa timu ya Zanzibar Islands , Fahad na Captain wa Timu ya Tanzania Dula , kombe ambalo timu zao zitashuka dimbani siku ya Jumapili ya Tarehe 02/06/2013, ambapo katika kuchezesha Droo ya michuano hiyo timu za Zanzibar na Tanzania Bara zimepangwa kukutana katika mchezo wa fungua dimba hapo kesho.
 Balozi akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Timu zetu na Baadhi ya Vijana wachezaji, baada ya kuwakabidhi Kombe na Bendera ya Tanzania itakayopepea kwenye mashindano hayo kuanzia tarehe 01/06/2013 katika viwanja vya Memorial Grounds , Forest gate  na Fainali kuwa tarehe 15/06/2013 katika Uwanja wa Westham Football Grounds (Upton Park ).
 Balozi Kallaghe akiwa katika picha ya pamoja na Waandaaji wa Shindano hilo litakaloundanisha timu za Nchi 20 za jamii ya Africa wanaoishi Uingereza. Pichani vilevile ni baadhi ya Viongozi wa Timu zetu za Tanzania na Zanzibar islands.
WATANZANIA WOTE MNAOMBWA MJITOKEZE KWA WINGI KATIKA KUSHANGILIA TIMU ZETU . MASHINDANO YANAANZA JUMAMOSI HII
 TAREHE 01/06/2013 kwenye MEMORIAL PARK GROUNDS , East London,
TUNAWATAKIA KILA LA KHERI TIMU ZOTE KOMBE LIRUDI UBALOZINI KUTOKA KATIKA TIMU MOJAWAPO YA JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...