Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, June 1, 2013

BIGRIGHT KUHAMASISHA MASUMBWI


kampuni iliyojitolea kuinua vipaji vya michezo nchini ya Bigright promotion, katika kuusambaza mchezo wa masumbwi nchini imeandaa mchezo mwingine kibaha-picha ya ndege kwa kuwakutanisha mabondia wakali wa eneo hilo la pichayandege  na wale waishio mjini ambao mara kwa mara hupata kucheza michezo mingi tofauti na vijana walio nje ya mji kama hao wa picha ya ndege.

Akilizungumzia pambano hilo Ibrahim kamwe, ambae pia ni katibu wa ngumi za kulipwa nchini na ndie anaeratibu mapambano hayo alisema huo ni mkakati aliouanzisha akianzia kwa lile pambano la chalinze mwezi uliopita na tarehe 25/5/2013 hili hapa la kibaha, litafuatia la tarehe 9/5/2013 kule bagamoyo na mapambano mengine yatakayo tangazwa hapo baadae tarehe ikiwa imeshapangwa.
hapo kibaha picha ya ndege tunategemea kuwachezesha GODWIN KEVIN wa pichaya ndege na saleh mkalekwa wa Dar es salaam,nae bondia machachali anaechipukia kwa kasi ambae bado hajapoteza pambano hata moja bondia toka kibaha mwenye mwili mkubwa na maguvu mengi ZUMBA KUKWE atazipiga na jofrey katili toka dar mapambano hayo ni ya raundi nanenane,pia kutakuwepo na mapambano mengine mengi ya utangulizi na ngumi zinategemewa kuanza saa kumi jioni katika ukumbi wa CCM hall hapohapo picha ya ndege.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...