Taarifa kwa vyombo vya habari
Wanachama Yanga, Simba waaswa kulipia ada kupitia M-pesa.
Dar es Salaam (3 January
2013) –Kutokana na kukua kwa kasi kwa maendeleo ya teknolojia katika sekta ya
soka nchini –klabu zinazoshiriki ligi kuu Tanzania bara zimeaswa
kuwahamasisha wanachama wa klabu hizo kulipia ada ya uanachama kupitia huduma
ya M -Pesa.
Mkuu wa Masoko wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa, alisema
kuwa hali hiyo itasaidia kuepusha ubebaji wa fedha taslimu mbali na hivyo, pia
zoezi hilo liitapunguza upotevu wa muda wa wanachama kutoka sehemu moja hadi
nyingine na kwenda klabuni kulipia ada ya uanachama.
“Iwapo vilabu vya soka nchini vitawaahamasisha wanachama
wake kutumia huduma ya M-Pesa kulipia
ada ya uanachama wataweza kuoka muda wa kwenda klabuni, wataokoa gharama na pia
kutakuwa na usalama wa fedha zao,” Bw. Twissa alisema.
Aidha, Bw. Twissa aliongeza kuwa kutokana na utumiaji wa
malipo kwa huduma ya M-Pesa –mapato ya vilabu pia yatakuwa salama.
Hivi karibuni mhasibu wa klabu ya soka ya Simba, alivamiwa
na kuporwa fedha za mapato ya klabu hiyo zilizotokana na mgawo wao wa mechi ya
kirafiki kati ya klabu hiyo na klabu ya Tusker ya Kenya.
Bw. Twissa, anaamini kuwa kwa kuanzishwa kwa huduma hiyo ya
ulipaji wa ada ya uanachama kwa vilabu kwa kupitia huduma ya M-Pesa itasadia
kuchochea ongezeko la idadi ya wanachama kwenye vilabu hivyo pamoja na uhai wa
wanachama hao.
“Huduma hii ya M-Pesa nina imani itakapoanza itasaidia
kuongeza idadi ya wanachama wapya kwenye vilabu na hata kuongeza mapato ya
vilabu. Kuna wanachama wengine ambao wanashughuli nyingi ambapo kwao kupata ule
muda wa kufanya mambo kama hayo ni nadra sana
lakini pia kuna wengine wao wanapata uvivu wa kwenda kulipia ada hiyo,”
alisema.
Huduma ya M-Pesa nchini imekuwa ikikuawa kwa kasi ambapo
imeweza kurahisisha maisha ya wananchi kwa ujumla kwa kupata mahitaji ya kila
siku ya binadamu. Hivi karibuni, Vodacom Tanzania imeingia mikataba na
Shoppers Supermarket kwenye maeneo ya Msasani na Masaki.
No comments:
Post a Comment