MBUNGE wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe Deo Filikunjombe (pichani)awalipua watumishi wa idara ya maji katika Halmashauri ya wilaya ya Ludewa akidai wanachelewesha mradi wa maji hivyo wanataka kumchonganisha na wapiga kura wake wa kijiji cha Maholong'wa kata ya Ludende ili akose kura mwaka 2015.
Akizungumza
jana kwa jazba katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo
mbunge Filikunjombe ambae alilazimika kumsimamisha mwakilishi wa
mhandisi wa maji wilaya ya Ludewa Teudelin Mfute aliyemwakilisha
mhandisi wa maji wilaya ya Ludewa vijijini ,ili aeleze sababu ya
kuendelea kuchelewesha mradi huo wakati tayari serikali imetoa fedha
kwa ajili
ya kuanza mradi huo.
"Nataka
unieleze mhandisi wa maji madunda kuna maji hakuna maji ....sasa kama
Madunga unasema hakuna maji Maholong'wa watapataje maji ...sasa
watendaji wa Halmashauri mliopo hapa naomba hi mtaniwia radhi kuwa
idara ya maji Ludewa kuna shida ila nawahakikishia kuwa tutakaa
tutalimaliza"
Alisema
haiwezekani wananchi wanatabika na kulia juu ya ukosefu wa maji
huku watendaji wa serikali wakiendelea kukaa maofisini huku
wakilipwa pesa bila kufanya kazi .
Filikunjombe
alisema lazima atahakikisha kila mtumishi wa umma katika wilaya hiyo
ya Ludewa anatimiza wajibu wake kwa kuwajibika kwa wananchi badala
ya kuendelea kukaa ofisini ,hivyo aliwataka idara ya maji wilaya ya
Ludewa kujitathini kabla ya kuwajibishwa .
Kwani
alisema
kuwa idara hiyo mbali ya kushindwa kuwajibika kutimiza wajibu wake
bado katika kijiji hicho amejitokeza mhisani kwa ajili ya kusaidia
mradi huo na kuwaomba idara hiyo ramani kwa ajili ya kuanza
utekelezaji wa mradi huo ila bado wameshindwa kuchora mchoro huo hadi
sasa kwa zaidi ya miezi sita sasa.
"Nimezungumza
na Mladea ambao ndio wahisani wanadai hadi sasa bado hawajapata
mchoro huo ....nimezungumza na watu wa idara hiyo wanadai kuwa bado
mchoro huo ....naomba mfikishia salamu zangu mhandisi wa
maji vijijini kuwa mimi kama mbunge na wananchi wa kata ya Ludende
hatujafurahishwa na utendaji kazi yenu "
Alisema
kuwa wananchi hao hadi sasa wamepata kuchangia fedha kwa ajili ya
mradi huo wa maji kiasi cha shilingi 10,000 kila mmoja na wapo
tayari kujitolea kuchimba mitaro ya kupitisha bomba ila watendaji
wa idara hiyo ya maji wamekuwa kikwazo kikubwa .
Kwa
upande wao wananchi wa kijiji hicho cha Maholong'wa wamempongeza
mbunge huyo kwa kubaini uozo huo wa watendaji wa idara hiyo ya maji
wilaya ya Ludewa na kuwa wao toka nchi ipate uhuru hawajapata kuona
wala kutumia huduma ya maji safi ya bomba zaidi ya kuendelea kutumia
maji ya mabondeni na madimbwi ya mvua ambayo si safi na salama kwa afya
zao.
Walisema
kuwa awali walianza kumchukia
mbunge huyo amoja na diwani wao kwa kuwaona kama mataeli na hata
wanaoitisha mikutano walikuwa wakishindwa kufika kutokana na kuona
kama wamedanganywa katika mradi huo ila sasa wamebaini kuwa watumishi
hao wa idara hiyo ya maji ni kikwazo na wao tayari kuungana na mbunge
wao kutaka wafukuzwe katika halmashauri hiyo kwa madia kuwa si
msaada kwao.
No comments:
Post a Comment