Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, January 8, 2013

ZANZIBAR YAZINDUA MITAMBO YA GIJITALI LEO.


Jengo la Mradi wa Kuhama kutoka Teknolojia ya Analojia kwenda Digital lililojengwa eneo la Rahaleo Mjini Zanzibar, baada ya kuzinduliwa rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohammed Shein, ikiwa ni shamra shamra  za kuaadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
 Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Agape Association LTD, Dr Vernon Fernandes, (kushoto)  akitoa maelezo ya namna mtambo wa Dijitali unavyofanya kazi kwa Rais wa Zanzibar baada ya kufanya uzinduzi wa  Mradi wa Kuhama kutoka Teknolojia ya Analojia kwenda Dijital  Rahaleo Mjini Zanzibar leo, ikiwa ni shamra shamra  za kuaadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, (kulia) Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Said Ali Mbarouk, na (watatu kulia) Dk.Anny Fernandes.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akifunua panzia kufungua jengo la Mradi wa Kuhama kutoka Teknolojia ya Analojia kwenda Digital Rahaleo Mjini Zanzibar, ikiwa ni shamra shamra  za kuaadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Agape Association LTD, Dr Vernon Fernandes, (kulia) baada ya kufanya uzinduzi wa  Mradi wa kuhama kutoka Teknolojia ya Analojia kwenda Dijital akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar.
Baadhi ya Viongozi wa Kampuni ya AgapeAssociation,LTD na wananchi wakimsikiliza Rais Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, alipokuwa akizungumza nao katika jengo la  Studio ya kurikodia Sanaa na Muziki ambalo lilifanyiwa ukarabati na kurejeshwa hadhi yake, ikiwa ni shamr shamra  zakuaadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akikata utepe kufungua jengo la Mradi wa Kuhama kutoka Teknolojia ya Analojia kwenda Digital hapo Rahaleo Mjini Zanzibar,ikiwa ni shamra shamra  za kuaadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi  ya Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...