MSANII nyota wa miondoko ya Mchiriku, Omari Omari, aliyefariki leo afajiri atazikwa kesho saa 7 mchana. Kwa mujibu wa King Sapeto, rafiki wa karibu wa marehemu, mazishi
yatafanyika Temeke Mikoroshini jijin iDar es Salaam na kuanzia leo ndugu
na jamaa wa marehemu wanategemea ujumbe mzito kutoka kwa viongozi wa
Serikali watakaopishana kwenda kutoa mkono wa faraja kwenye nyumba ya
msiba.
Kwa siku za hivi karibuni viongozi wa serikali na vyama mbali mbali
vya siasa wamekuwa mstari wa mbele kwa kushiriki bega kwa bega kwenye
misiba ya wasanii, hivyo watu wa karibu na Omari Omari wanategemea hali
hiyo pia itatokea kwa ndugu yao kipenzi. "Hatutegemi ubaguzi wa misiba"
anaeleza mmoja wa ndugu wa marehemu.
Omari Omari aliyetamba na wimbo “Kupata Majaaliwa” ndani yake kukiwa
na mstari mkali unaosema ndefu amekosa ng’ombe lakini mbuzi kapewa,
alifariki katika hospitali kuu ya Temeke baada ya kuugua ugonjwa wa
kifua kikuu.
Msiba uko Temeke Mikoroshini nyumbani kwa baba yake.
MUNGU AMLAZE MAHALA PEMBA PEPONI AMIN
No comments:
Post a Comment