KUZIMIA, Mama ambaye jina lake halikufahamika alizimia Bommoabomoa Dodoma.
Mwananchi aliyekuwa na silaha kwenye eneo la bomoabomoa.
Bomoa nyumba Njedengwa Dodoma Oktoba 2011
majeruhi wa Njedengwa Dodoma Oktoba 2011. 5
waandishi wa habari walivyoonja adha ya Mabomu.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
DIWANI wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kata ya Makulu mkoani Dodoma
Ally Biringi, amekirushia Makombora Mazito Chama cha Mapinduzi (CCM)
mkoani humo akikituhumu kuwa kinajichanganya na kujikaanga kwa mafuta
yake kwa ubaguzi wa Kiitikadi katika kuwahudumia raia wake.
Biringi
alisema hayo jana kufuatia Kauli ya CCM dhidi ya wapangaji wa Kaya zaidi
ya 100 zenye wakazi takribani 1,044 wa Kata ya Kikuyu inayotawaliwa na
CCM, waliopanga kwenye nyumba za Mamlaka ya Ustawishaji Makao Mkuu
(CDA), waliotakiwa kuhamishwa kwa nguvu Alhamisi, Februari 28, 2013.
Akizungumzia
tuhuma hizo Biringi ambaye wananchi humuita Kiboko cha Yusuf Makamba
alisema, CCM kinajichanganya kinafanya Siasa na Usanii kwenye Haki za
Wananchi wake, ambapo Katibu Mkuu wake wa Mkoa wa Dodoma Albert Mgumba
alipoongea na Wandishi na kusema CCM inaishauri Serikali na CDA itumie
Busara na Hekima suala la kuwahamisha kwa nguvu wapangaji hao.
“Sipingi kauli
ya kutumia Hekima, Busara kuwahamisha wapangaji ndicho Serikali na CDA
inavyotakiwa ifanye, ila CCM haikutoa kauli ya namna hiyo bomoabomoa ya
Njedengwa kwa wananchi wa Kata yangu Oktoba 2011, walipigwa Mabomu,
kuharibiwa mali na Damu kumwagwa ili kumfurahisha mwekezaji”.
Biringi
alisema, Mioyo ya Wananchi walioko kwenye Maeneo na Kata za CCM ni sawa
na Mioyo ya wananchi walioko kwenye maeneo yanayotawaliwa na vyama vyote
vya upinzani kikiwemo Chadema, hivyo wote wana fursa sawa ya kutendewa
haki kama unavyokata msumeno.
Aidha alisema,
kitendo cha CCM kuinua mdogo na kupaza sauti ya utetezi pale tu ambapo
utawala uliopo ni wa Chama chake na kuwa likizo maeneo ambayo
yanatawaliwa na upinzani, hali hiyo inatafsirika kama ni ubaguzi wa
kiitikadi.
No comments:
Post a Comment