Rais Jakaya Kikwete akiangalia shughuli za uzalishaji umeme hivi karibuni, baada ya vutanikuvute ya muda mrewfu Serikali imeamua kujenga kiwanda cha gesi mkoani Mtwara |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,
Eliakim Maswi alisema jana kuwa ujenzi huo unaofanywa na Kampuni ya
China Petroleum and Technology Development Co-operation (CPTDC), ambao
awali, ulipaswa kuanza wiki iliyopita, umeanza juzi baada ya Serikali
kufikia mwafaka na wananchi wa Kijiji cha Msimbati kinapojengwa.
“Mkuu wa Wilaya ya Mtwara (Wilman Ndile) na vijana
wake walilazimika kufika Kijiji cha Msimbati, ambako wananchi walikuwa
na mgogoro na watu wa Marine Park,” alisema Maswi.
Alisema baada ya ziara hiyo kushindwa kufanyika
Jumapili iliyopita, uongozi wa wilaya ulikutana na viongozi wa kijiji na
kufikia mwafaka uliofanikisha kuanza kwa ujenzi huo.
Alisema kuanzia mradi huo kutatoa ajira za kawaida
kwa wakazi saba wa maeneo yanayozunguka mradi huo na kwamba kazi hiyo
itaongeza mahitaji ya bidhaa mbalimbali na huduma katika Kata ya
Msimbati
“Mathalan kuku, matunda na mboga za majani
vinahitajika sana. Sasa wananchi ambao awali, hawakutaka kuelezwa
lolote, wameanza kuchangamkia fursa hizo jambo ambalo litawanufaisha
zaidi,” alisema.
Ujenzi huo ulielezwa kuwa unatekelezwa sambamba na mwekezaji kujenga visima vitatu vya maji safi na salama kijijini Madimba.
Alisema mwekezaji pia atasambaza umeme kwa kaya
300 za ndani na jirani ya kijiji hicho na kwamba vifaa vitakavyotumika
katika kazi hiyo vinatarajiwa kuwasili mwishoni mwa mwezi huu.
Maswi alisema shule zote kwenye Kata ya Msimbati
kikiwamo Kijiji cha Madimba, zitakarabatiwa na mwekezaji huyo ikiwa ni
sehemu ya mpango wa wananchi waishio maeneo ya mradi kunufaika na
uwekezaji.
Hata hivyo, habari nyingine zinaeleza kuwa ulinzi
umeimarishwa katika eneo hilo la mradi ili kuhakikisha hali ya usalama
inaendelea kuwapo.
Mgawo wa umeme
Akizungumzia kuhusu kukatika mara kwa mara kwa umeme katika maeneo mengi nchini hali inayowafanya wananchi kuamini kuwa kuna mgawo wa umeme kinyemela, Maswi alisema kamwe Taifa halitaingia gizani.
Akizungumzia kuhusu kukatika mara kwa mara kwa umeme katika maeneo mengi nchini hali inayowafanya wananchi kuamini kuwa kuna mgawo wa umeme kinyemela, Maswi alisema kamwe Taifa halitaingia gizani.
Alisema kukatika kunakotokea sasa kumesababishwa
na kazi za kiufundi zilizotarajiwa kukamilika jana jioni... “Kwa taarifa
nilizonazo, mtambo mdogo uliopo Ubungo unabadilishwa na kuwekwa mkubwa,
pia Kipawa kuna matengenezo ya transfoma ili kuwezesha usambazaji wa
umeme hadi Kisarawe na nyie mnaweza kwenda mkashuhudia kinachoendelea.”
No comments:
Post a Comment