Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, June 1, 2013

NEY WA MITEGO: NDOA ZINASHUSHA KIWANGO CHA MSANII


Na Elizabeth John

MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Emmanuel Elibriki ‘Ney wa Mitego’ amesema asilimia kubwa ya wasanii ambao wanashuka kimuziki ni wale ambao wanakua wameingia katika maswala ya ndoa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Ney alisema wasanii wengi wa bongo wanakurupuka katika hilo na ikitokea ambaye amejipanga ni wachache sana na hapa bongo hajaona.

“Wasanii wengi wa bongo tunakurupuka na hatujipangi katika mambo ya familia zetu na ndio maan aikitokea msanii anaoa basi ujue lazima atashuka kimuziki,” alisema Ney.

Katika hatua nyingine, mkali huyo alimpongeza msanii mwenzake, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinum’ kwa kuwa na mpango wa kuoa hivi karibuni.

“Diamond ni mdogo wangu, nampa hongera kwa kutaka kuingia katika maisha ya ndoa hilo sio swala dogo namuombea afanikishe mipango hiyo,” alisema.

Diamond ametangaza kwamba anatarajia kufunga ndoa miezi miwili ijayo na kusema kwamba anaamini kwa kufanyahivyo utakua ni hatua moja wapo ya kuzidi kufanikiwa kimaisha.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...