Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, June 1, 2013

MH. DEWJI AMWAGA MISAADA KATIKA JIMBO LA SINGIDA YENYE THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 87 NA KUWATAKA VIONGOZI KUTEKELEZA ILANI ZA CCM.




E83A0131
Picha juu na chini ni Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mh. Mohammed Gullam Dewji akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kituo cha mabasi cha zamani mjini Singida.
E83A0138
E83A0112
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara ulioitishwa kwa ajili ya mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji kuzungumza na wananchi wa jimbo lake.
E83A0094
Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mh. Mohammed Gullam Dewji, akiwa anasalimiana na Wana CCM na wananchi wa Singida mjini kwenye kituo cha mabasi cha zamani mjini Singida.Picha zote na Nathaniel Limu
--
Na Nathaniel Limu.
Mbunge wa Singida mjini (CCM) Mh. Mohammed Gullam Dewji amemwaga misaada mbalimbali ikiwemo kuwaongezea mitaji wauza kahawa chungu, ambayo haijawahi kutolewa jimboni humo na mbunge au mfadhili yeyote kwa wakati mmoja, kabla na baada ya Tanzania kupata uhuru.
Misaada hiyo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 87.9, ni pamoja na mabati 100 na mifuko ya saruji 100, kwa kila shule 17 za sekondari jimboni humo.
Misaada mingine ni vyereheni viwili kwa kila kata 19 na cherehani moja kwa kila tawi la CCM jimboni humo.
Pia vikundi 16 vya wajasiriamali vikiwemo vya kung’arisha viatu, mafundi baiskeli, wapiga debe wa vituo vya mabasi, wasukuma matoroli, wakereketwa wa mashina ya CCM, watengeneza viatu vya kienyeji na baba, mama lishe, kila kimoja kimeongezewa mtaji wa shilingi 500,000 taslimu.
Vifaa hivyo na mitaji ya biashara, vimetolewa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kituo cha zamani cha mabasi mjini Singida.
Akizungumza kwenye mkutano huo wa hadhara uliohudhuriwa na maelfu ya wana-CCM na wananchi kwa ujumla, Mh. Dewji amesema msaada huo ni mwendelezo wa misaada yake anayoitoa kwa ajili ya kuiunga mkono serikali katika kuwatumikia wananchi.Amesema pia kuwa misaada hiyo ni sehemu yake ya utekelezaji wa ilani ya CCM katika kuwatumikia wananchi wa jimbo la Singida mjini.
Amesema “Tunatakiwa tujitume usiku na mchana, ili tuhakikishe kila tuliyoyaahidi kwenye ilani yetu, yote tumeyakamilisha, vinginevyo wananchi hawatatuelewa. Wananchi wanahitaji utimilifu wa ahadi na sio uhodari wa kujieleza kwenye majukwaa”.
Katika hatua nyingine, Mh. Dewji ametumia fursa hiyo kuwaomba viongozi na watendaji kuendelea na moyo safi wa kuwatumikia wananchi bila kuchoka.
Amesema pia wawe waaminifu na waadilifu kwa wananchi na waongozwe kwa dhamira iliyo njema, yenye uzalendo wa kuipenda nchi yetu na watu wake.
Mbunge Dewji amesema “Tuendelee kuhubiri amani na utulivu kwenye majukwaa, wakati wote tuwaelekeze wananchi kwenye kujiletea maendeleo endelevu ya wakati huu na wakati ujao”.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...