BINGWA wa ngumi za kulipwa anayetambuliwa na vyama vya ICB, IBF na WBC,
Francis Cheka 'SMG' usiku wa kuamkia leo amedhihirisha kwamba hana
mpinzani katika ngumi hizo nchini baada ya kumchapa kwa KO mpinzani wake
mkubwa, Karama Nyilawila na kuongeza taji jingine.
Cheka alimpiga Nyilawila katika raundi ya sita ya pam,bano hilo
lililokuwa la uzani wa Super

lililokuwa la uzani wa Super Middle la raundi 12 lililofanyika kwenye
ukumbi wa PTA, Temeke jijini Dar es Salaam na kutwaa ubingwa wa Mabara
wa UBO uliokuwa wazi.
Pambano hilo lililohudhuriwa na mashabiki lukuki, lilishuhudia raundi
zote tano za kwanza Nyilawila akionyesha kumdhibiti Cheka kwa kumchezea
'kibabe' akitumia nguvu nyingi kujihami na baadhi ya watu ukumbini
kuamini mwisho wa tambo za Cheka zilikuwa zimewadia.
Hata hivyo raudni ya sita ilipoanza Cheka alionyesha amebadilika na hasa
baada ya kocha wake Abdallahj Saleh 'Komando' kupanda ulingoni na
kuzungumza na bondia huyo na kumshushia kipigo Nyilawila, ambapo moja ya
makonde matatu ya mfululizo yalimpeleka chini mpinzani wake.
Mwamuzi wa pambano hilo, Jerome Waluza alimhesabia Nyilawila ambaye
alijitahidi kuinuka, lakini ghafla akaonyesha ishara kwamba asingeweza
kuendelea na pambano hilo na ukumbi mzima kuripuka kwa shangwe
akishangiliwa Cheka ambaye hiyo ni mara ya pili kumpiga Nyilawila.
Kabla ya pambano hilo lililoanza majira ya saa 3;40 usiku, kulikuwa na
mapambano saba ya utangulizi pamoja na burudani ya muziki toka bendi ya
Mashujaa ambao hata hivyo sio wapenzi wengi walioweza kuishuhudia
kutokana na kuondoka ukumbini mapema.
Katika pambano la kwanza la utangulizi Said Mbelwa alimpiga kwa pointi
Dickson Mwakipesile, Juma Kihiyo alipigwa kwa pointi na Ibrahim Mahokola
katika pambano lililovutia kwa namna mabondia hao walivyoonyeshana
kazi.
Pia mdogo wa Cheka, Cosmas Cheka alifanikiwa kuibuka na ushindi wa
pointi dhidi ya Fadhil Awadh katika pamnbano jingine lililosisimua wengi
kwa ufundi uliokuwa ukionyesha na mabondia hao, naye Shaaban
Kilumbelumbe alimpiga kwa pointi Anthony Mathias kabla ya Safari Mbiyu
kumpiga kwa KO ya raundi ya kwanza Khalfan Jumanne.
Michezo minginme iliwakutanisha Stan Kessy na Seba Temba, pambano
lililoisha kwa mabondia hao kutoka sare na Hassani Kidebe alitolewa
nishai na Deo Samwel kwa kupigwa kwa pointi.
Mgeni rasmi katika pambano hilo alikuwa Kamanda wa Polisi Kanda maalum
ya Dar es Salaam ambaye aliutangazia umma kwamba kama Mlezi wa Ngumi za
Kulipwa amefanikiwa kuwafuta wafadhili katika mchezo huo na
kumtambulisha raia mmoja wa kigeni kwamba ni miongoni mwao.
Middle la raundi 12 lililofanyika kwenye