KAMPUNI YA KUSAFIRISHA MIZIGO YA SERENGETI FREIGHT FORWARDERS LTD YAKABIDHI MSAADA WA VITU MBALIMBALI VILIVYOTOLEWA NA WATANZANIA WAISHIO UINGEREZA KUWASAIDIA WAKAZI WA MABWEPANDE
Mkuu
wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (kulia) akipokea msaada wa
vitu mbalimbali vilivyotolewa na watanzania waishio nchini Uingereza
kuwasaidia wakazi wa Mabwepande walioathiriwa na mafuriko yaliyotokea
mwezi Desemba 2011 jijini Dar es salaam leo. Wanaokabidhi msaada huo ni
kutoka kushoto ni Awadh Salim mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Bw. Mohammed
Abdulrahaman Meneja wa kampuni hiyo Tanzania na Bw. Chris Lukosi,
Mkurugenzi wa Kampuni ya Usafrishaji wa Mizigo ya Serengeti.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Usafrishaji wa Mizigo ya Serengeti (Serengeti Freight
Forwarders Ltd) Bw. Chris Lukosi akimkabidhi Mkuu wa mkoa wa Dar es
salaam Saidi Meck Sadiki (kulia) moja ya boksi lenye vitu mbalimbali
vilivyotolewa na watanzania waishio nchini Uingereza kuwasaidia wakazi
wa Mabwepande walioathiriwa na mafuriko yaliyotokea mwezi Desemba 2011
jijini Dar es salaam.
Mkuu
wa mkoa wa Dar es salaam akiwaeleza jambo viongozi wa Kampuni ya
Usafirishaji wa Mizigo ya Serengeti (Serengeti Freight Forwarders Ltd)
iliyosafirisha bure msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo viatu, nguo na
vifaa vya watoto vilivyotolewa na watanzania waishio nchini Uingereza
kuwasaidia wakazi wa mabwepande.
No comments:
Post a Comment