Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, September 19, 2012

JACKLINE WOLPER AJIBU MAPIGO YA IRENE UWOYA, ASEMA NA YEYE HANA MPANGO HUO! SABABU!? SOMA ZAIDI HAPA...




Jackline Wolper


BAADA ya msanii Irene Uwoya kudai kuwa msanii mwenzake Jackline Wolper hana kiwango cha kuweza kushiriki naye kwenye filamu moja, naye Wolper amejibu mapigo kuwa hata yeye haitaji kucheza naye kwani anaamini kiwango chake si cha mdomoni bali mara zote anakionesha akiwa kazini na hata mashabiki zake wanajua hilo

Jitihada za kutafuta Wolper ambaye mara kadhaa simu yake ilikuwa imezimwa na baada kupatikana msanii huyo alidai yuko bize ambapo aliamua kumtumia rafiki yake wa karibu ili kujibu hoja, ambapo alidai kuwa hawezi kuzungumza chochote kwani wanaosema yeye hana kiwango hawamjui na wanamuona juu juu lakini hawajawahi kushiriki naye kwenye kazi ambayo inaweza kutoa majibu yote.


Rafiki huyo ambaye hata hivyo alikaa kujitambulisha jina, alidai alichoambiwa akijibu ndicho anachokitoa, ambapo aliongeza kuwa kauli ya Uwoya haimshtui na ataendelea kusimama imara katika kila kazi anayotoa kwa lengo kuwapa ujumbe mashabiki wke.


“Kwangu siwezi kujibu kauli za mtu ambaye hana uwelewa wa nini anachikisema najua ni kwamba wanaoweza kutoa kauli kama hizo ni mashabiki na wapenzi wa kazi zetu, hivyo nawaomba wadau wa wangu wasimsikilize mtu ambaye anakaribia kupotea kwenye tasnia”.

Hata hivyo baada ya kuachana na rafiki huyo chanzo cha habari kilizungumza tena na Wolper, ishu iliibuka upya ni kwamba baada ya kudaiwa kuwa wameachana na mpenzi wake Dallas na amepokonywa mkoko wa wenye thamani ya sh. mil. 175, alikana habari hizo na kudai kuwa yeye mwenyewe hajatamkiwa kuwa ameachwa. “Hizo habari hazina ukweli si unajua watu wakiamua kutoa ishu za uongo wanatoa ili tu mtu aonekana mbaya, lakini najua nafasi yangu ni ipi ” alidai Wolper.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...