■AINGIA KWA MBEMBWE ZA AINA YAKE
■AKATAA KUKUMBATIANA NA WAGENI WAKE UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA HOSEA KUTAKO, WINDHOEK, NAMIBIA
BONDIA
Mtanzania, Rajabu Maoja, amelitingisha jiji la Windhoek, nchini
Namibia, alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Hosea Kutako.
Maoja
aliingia kwa mbemwe za aina yake na kugoma kukumbatiana na wenyeji wake
ambao walikuwa na shahuku kubwa ya kumlaki wakati wa mapokezi yake kwa
kumkumbatia.
Akiwa
na sura ya kujiamini huku akitembea kibabe Mtanzania Maoja, alionyesha
nia ya kuuchukua mkanda wa ubingwa wa IBF katika bara la Afrika wakati
atakapoumana na bingwa wa Namibia Gottlieb Ndokosho kesho siku ya
Jumamosi.
Mpambano
huo ulipewa jina la Vita Vya Jangwa wa Kalahari (The Battle for the
Kalahari Desert) na waandaaji wake ambao ni kampuni ya Kinda Boxing
Promotions inayoongozwa na Simon Nangolo limeleta shamrashamra za aina
ya pekee katika ukanda huu wa Kusini mwa jangwa la Sahara.
Mpambano
huo ni moja ya mapambano ambayo yapo kwenye programu ya Utalii wa
Michezo ya IBF (IBF Sports Tourism) ambayo inasimamiwa na Shirikisho la
Ngumi la Kimataifa (IBF) na kuratibiwa na Rais wa IBF katika bara la
Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi, Mtanzania Onesmo Alfred
McBride Ngowi.
Nao
mabondia kutoka Zimbabwe na Afrika ya Kusini ambao watacheza mapambano
ya awali wameshafika na tayari shamrashamra za mpambano huo zimeshika
kasi kwa wadau na wapenzi wa ngumi wa nchi ya Namibia na nchi jirani
kama Botswana, Afrika ya Kusini, Lesotho na Swaziland.
Hii ni mara ya kwanza kwa ushandani mkubwa namna hiyo kuwahi kutokea katika jiji la Windhoek hapa Namibia.
Mpizania wa Maoja Gottlieb Ndokosho ameingai mitini na hajaonekana tangu tuingie katika jiji hili la maraha!
Kesho ni kesho na Watanzania wamuombee mwakilishi wao ili aweze kuipeperusha vizuri bendera ya Tanzania!
Mungu mbariki Rajabu Jumanne Maoja, Mungu ibariki nchi nzuri ya Tanzania.
Imetolewa na: Uongozi
Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC)
No comments:
Post a Comment