Mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara, kesho inaingia raundi ya nne, ambapo kwa mechi za Super Weekend
ambazo zitakuwa zikionyeshwa moja kwa moja (live) na kituo cha
televisheni cha SuperSport cha Afrika Kusini.
Miongoni mwa mechi zitakazoonyeshwa
na kituo hicho, mechi ya kwanza itakuwa ni kati ya Azam na JKT Ruvu
Stars, itakayochezwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,
ambayo itaanza saa 1 kamili usiku kwa viingilio vya sh. 3,000 mzunguko,
sh. 5,000 kwa VIP C na VIP B wakati VIP A kiingilio kitakuwa ni sh.
10,000.
Jumamosi pia kutakuwa na mechi kati
ya Simba na Tanzania Prisons, ambayo pia itachezwa kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 11 kamili jioni na siku ya jumapili,
Yanga na African Lyon zote za jijini Dar es Salaam, zitakutana katika
uwanja huo huo kuanzia saa 11 kamili jioni.
Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam wenyewe utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar, mchezo utakaochezwa Oktoba 1, mwaka huu kuanza saa 10.30 jioni.
Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam wenyewe utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar, mchezo utakaochezwa Oktoba 1, mwaka huu kuanza saa 10.30 jioni.
Na mechi ya mwisho ya Super Weekend
itachezwa Oktoba 3 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
ikizikutanisha Yanga na Simba kuanzia saa 1 kamili usiku.
No comments:
Post a Comment