“Kama unataka kufanya vema kwenye mashindano yote unayoshiriki,
wachezaji wanapaswa kubadilishwa. Ndicho kitachotokea, kwamba mchezaji muhimu
kikosini anaweza kukalia benchi”
KOCHA Roberto Mancini wa Manchester
City amewaonya nyota wake na kuwaambia
hakuna aliye na namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha mabingwa hao wa
Ligi Kuu ya England.
Mancini amesisitiza kuwa, anaweza kumshusha yeyote kikosini
miongoni mwa wakali wake walioigharimu timu mabilioni ya fedha, kama njia kuu
ya mabingwa hao wa England
kupigania ushindi katika mataji manne wanayowania.
Mancini alisema: “Kama
unataka kwenda sawa katika mashindano yote unayoshiriki, unatakiwa kufahamu
kuwa wachezaji wanapaswa kubadilishwa.
“Ndicho kinachoweza kutokea, kwamba mchezaji muhimu na nyota
kikosini anaweza kukalia benchi kutii mahitaji ya mechi husika.”
Mancini alipigwa butwaa baada ya kikosi chake kupoteza
uongozi wa 2-1 hadi dakika ya 87 na hatimaye kufungwa mabao 3-2 Jumanne kwenye
dimba la Santiago Bernabeu – walipocheza na wenyeji wao Real Madrid.
Mshambuliaji Mario Balotelli aliwekwa benchi katika mechi
hiyo na kuzua utata na sintofahamu kuhusu majaaliwa yake, huku akiwa na
uwezekano pia wa kubaki benchi tena kesho wanapoumana na Arsenal katika mechi ya
Ligi Kuu.
Mancini alikizungumzia kikosi chake cha kwanza dhidi ya Madrid: “Nilifanya
maamuzi bora kwa faida ya timu. Ulikuwa ni uteuzi wa kimbinu zaidi kwa sababu
nilitaka kubaki na washambuliaji waili kwenye benchi na watatu wangekuwa wengi
zaidi.”
Kocha huyo akajitetea kuwa Balotelli hakufanya vema vya
kutosha, wakati akisafiri na timu kwenda Hispania.
Mancini akaongeza: “Mario alikuwa amechukizwa, lakini
nadhani ni jambo la kawaida. Hakuna mchezaji ambaye atafurahi kuachwa bila
kucheza kwwenye Uwanja wa Bernabeu.”
Balotelli alianzishwa kwenye kikosi cha kwanza cha City
kilichoumana na Stoke wiki iliyopita, lakinia akaonesha kiwango kibovu katika
mechi hiyo iliyoisha kwa sare ya bao 1-1 na kumkera Mancini.
No comments:
Post a Comment