Na Elizabeth John
SHIRIKISHO
la ngumi za ridhaa Tanzania (BFT), limeunda kamati itakayosimamia
mashindano ya Taifa yanayotarajia kuanza kutimua vumbi leo, katika
Uwanja wa Ndani wa Taifa, ili kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika
kwa kiwango cha Kitaifa.
Akizungumza
jijini Dar es salaam, Katibu Mkuuu wa BTF, Makore Mashaga alisema
kamati hiyo imeundwa kwa kuwajumuisha wataalamu wa ufundi kutoka kamati
za BFT, mabondia wa zamani na wataalamu wa mipango na fedha kutoka
katika taasisi na mashirika ambayo yamekuwa mstari wa mbele kusaidia kwa
vitendo shughuli na matukio mbalimbali ya BFT.
Aliwataja
wajumbe ambao wameteuliwa kuunda kamati hiyo kuwa ni Andrew Kweyeyana
ambaye ndie Mwenyekiti wa kamati, Willy Issangura, Juma Suleiman, Remy
Ngabo na Mohamed Kasilamatwi.
Wengine
ni Said Omary, Anthony Mwang’onda, Joel Magori, Charles Jilaba na
Undule Mwampulo ambao wote hao waliweza kusaidia kwa namna moja au
nyingine kwa bondia pekee hapa nchini, Suleiman Kidunda kuweza kufuzu
mashindano ya Olimpiki yaliyomalizika hivi karibuni London, Uingereza.
“Jukumu
walilopewa ni kuhakikisha mashindano yanafanyika kwa kufuata taratibu
zote za zote za Chama cha Ngumi cha Dunia (AIBA) na kuhakikisha fedha za
kuendesha mashindano zinapatikana na majukumu ya kamati hiyo
yatamalizika baada ya kumalizika kwa mashindano hayo.
No comments:
Post a Comment