Meneja
Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw. Peter Fauel akifafanua ujio wa Super
Sport nchini Tanzania na kuipongeza TFF kwa kuonyesha ushirikiano na
kuwa Chaneli hiyo itaonyesha mechi tano za Ligi ya Tanzania kuanzia leo
Ijumaa hadi Jumatano Oktoba 3 mwaka 2012.
Mkuu
wa Super Sport barani Afrika Bw. Andre Venter akielezea furaha yake
kuja Tanzania na kupata fursa ya kulitangaza soka la Tanzania kimataifa
kupitia chaneli ya Super Sport amesema chaneli hiyo imechafanya kazi
katika nchi za Kenya na Uganda na Sasa ni wakati wa Tanzania kuonyesha
kiwango chake cha soka Kimataifa.
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini (TFF) Bw. Leordiga Tenga akitoa
nasaha zake wakati wa uzinduzi wa wiki ya Soka Tanzania ambapo amevitaka
vilabu vitakavyopata bahati ya kuonekana katika chaneli hiyo kuonyesha
kiwango cha soka la Tanzania na kuzingatia nidhamu haswa mechi ya Watani
wa Jadi Yanga na Simba ambao wanatambulika barani Afrika kama timu
zenye upinzani mkali.
Meneja
Masoko wa Multichoice Tanzania Bi. Furaha Samalu akifurahi jambo na
watangazaji wa kipindi cha Africa Soccer Show wakati wa halfa hiyo.
Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania Barbara Kambogi akitoa
ufafanuzi kwa waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo kuwa Super
Sport wakishirikiana na TFF wapo hapa nchini na kwa mara ya kwanza
wanaonyesha mechi za Ligi ikiwemo timu ambazo hata siku moja hazijawahi
kuonekana kwenye Chaneli ya Super Sport na kuwataka wachezaji wa timu
hizo kuonyesha uwezo wao kwa sababu ni fursa ya pekee kuonekana katika
nyanja ya Kimataifa. Aidha amewataka Watanzania ambao hawajaunganishwa
na DStv wafanye hima kununua ving'amuzi ili waweze kushuhudia mechi hizo
pamoja na chaneli nyinginezo zinazopatikana katika DStv.
Meneja
Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw. Peter Fauel akisalimiana na baadhi ya
wageni waalikwa katika hafla fupi ya uzinduzi wa wiki Soka Tanzania
iliyofanyika jijini Dar kwenye Hoteli ya Southern Sun.
Dada Levina kutoka Multichoice Tanzania anayetazama kamera akifurahi jambo na wadau.
Meneja fedha wa Multichoice Tanzania Bw. Senguti (kushoto) akiteta
jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw. Peter Fauel.
Baadhi ya Wadau wa michezo wakipata viburidisho wakati wa uzinduzi wa wiki ya soka Tanzania.
Mkurugenzi
Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw. Peter Fauel (katikati) katika tete- a
-tete na Rais wa TFF Bw. Leordiga Tenga na Mkuu wa Super Sport Afrika
Bw. Andre Venter.
No comments:
Post a Comment