Marquee
tangazo
Sunday, September 16, 2012
KUELEKEA UCHAGUZI 2015. CUF yafanya harambee jijini Dar, yakusanya Tsh.129294925Millioni, Ni kwaajili ya kuimarisha Chama Mikoani kupitia kampeni yake ya Dira ya Mabadiliko Mchaka Mchaka Mpaka Kieleweke.
Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi CUF Prof.Ibrahim Lipumba, akichangia fedha kwenye harambee iliyozinduliwa na Chama hicho leo kwenye viwanja vya Jangwani ambapo hadi mkutano unamalizika tayari walikua wameshachangisha zaidi ya Tsh129Millioni. Pesa hizo ni maalum kwaajili ya kuimarisha chama hicho ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mkuu wa 2015.
Mwenyekiti wa CUF Prof. Lipumba (katikati) akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Machano Hamis wakimuangalia Naibu Katibu Mkuu bara Julius Mtatiro wakati nayeye akitoa mchango wake kwa chama hicho kwaajili ya harakati za chama hivho zakueneza kampeni yake ya Dira ya Mabadiliko.
Baadhi ya wanachama wa chama hicho wakifuatilia hotuba za viongozi wao.
Wengine walichukua ujmbe wa mabango yanayomnadi mwenyekiti wao.
Wanachama wa chama hicho wakiwa kwenye foleni ya kuchangia pesa kwenye harambee hiyo.
Mmasai akiruka juu kucheza ngoma zakwao akifurahai nyimbo za Chama Cha CUF wakati wa harambee ya kuchangia chama hicho.
Wasanii wa kundi la Lama lama ambao kwenye uchaguzi wa 2010 walijiunga na CCM na sasa kurejea CUF wakitumbuiza kwenye mkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Prof. Lipumba akiwa amekumbatiana na mmoja wa walemavu waliojitokeza kuchangia harambee hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment