Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Waka Waka kutoka Uholanzi, Bill Carney akikabidhi taa inayotumia mwanga wa jua kwa mkazi wa kijiji cha Matetema, Hasina Juma katika hafla ambayo kampuni hiyo ilikabidhi msaada wa taa 400 zenye thamani ya sh milioni 25 kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (wa tatu kushoto) kwa ajili ya wanavijiji wa Matetema na Kichungwani visiwani humo mwishoni mwa wiki. (Na Mpiga Picha Wetu)
Na Mwandishi Wetu
MAKAMU
wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Iddi
ametoa shukurani kwa kampuni ya Taa zinazotumia mwanga wa jua ya Waka
Waka ya nchini Uholanzi kwa mchango wao kwa maendeleo ya watanzania wa
Visiwani na Bara.
Shukrani
hizo alizitoa wakati akipokea msaada wa taa zinazotumia nishati ya jua
400 zenye thamani ya Shs milioni 25 zilizotolewa na kampuni hiyo
inayotokea nchini Uholanzi kwa wakazi wa vijiji vya Matetema na
Kichungwani katika Jimbo la Kitope visiwani humo juzi.
Aliongeza
kuwa matumizi ya taa za jua yatasaidia sana kupunguza ghara za maisha
zinazotokana na matumizi ya mafuta hivyo ni maendeleo makubwa sana
visiwani huko.
Akizungumza
katika ghafla hiyo mmoja wa waanzilishi wa Kampuni hiyo, Maurits Groen
alisema ni ukweli usiopingika kuwa watu wengi katika Afrika wanatumia
vibatari ili kupata mwanga hivyo teknolojia hiyo itasaidia sana si tu
katika kuepuka gharama za manunuzi ya mafuta ya taa bali pia itasaidia
kuepukana na athari zinazotokana na moshi wa mafuta ya taa.
'Tunajua
kuwa wakati taa ikiwaka tunavuta hewa na moshi ambao unaweza kuumiza
mapafu, macho na ajali za moto hivyo matumizi ya taa hizo yatasaidia
kuepukana na athari hizo'.
Inakadiriwa
zaidi yaw atu bilioni 1.5 duniani kote huishi bila umeme wakitegemea
taa za mafuta huku watu milioni sita wakipata majeraha ya kuungua
yanayosababishwa na ajali za moto wa mafuta ya taa wakati watu milioni
780 wanawake kwa watoto huvuta hewa yenye uzito sawa na pakiti mbili za
sigara kwa siku.
No comments:
Post a Comment