Mwenyekiti na Afisa
Mtendaji Mkuu wa Chama Cha Madini na Nishati nchini Joseph Kahama akizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua mfululizo wa vipindi vine vya
televisheni vitakavyoonyeshwa kuanzia mwishoni mwa mwezi huu kutoa elimu juu ya
sekta ya madini nchini.
Baadhi ya wadau wa sekta ya madini nchini na waandishi wa
habari wakifuatilia kwa makin vipindi vya
televisheni vilivyotayarishwa na Chama
Cha Madini na Nishati nchini vitakavyoonyeshwa kuanzia mwishoni mwa mwezi huu
kutoa elimu juu ya sekta ya madini nchini, wakati wa uzinduzi wake jijini Dar es Salaaam
jana.
KATIKA kile kinachoonekana ni kuguswa na malalamiko na
maneno ya wananchi juu ya sekta ya madini nchini Chama Cha Madini na Nishati
nchini (TCMC) kimekuja na vipindi vya televisheni ili kutoa elimu juu ya namna
sekta hiyo inavyoendeshwa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa
vipindi hivyo jijini Dar es Salaam juzi Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa
TCME Joseph Kahama amesema wameona kwamba ipo haja yakuongeza uelewa kwa jamii
juu ya athari zake kwenye jamii kimazingira na uchumi.
Akifafanua zaidi kuhusu vipindi hivyo kahama alisema kuna
maeneo manne hasa ndiyo yatakayo gusiwa zaidi kwenye mfululizo wa vipindi hivyo
ambayo ni mguso wa madini tangu hatua za awali, mazingira na athari za
uchimbaji, mchango wa uchimbaji madini kwenye jamii na upanuaji na
ubadilishanaji wa ufahamu na ujuzi (na upanuzi wa wigo wa ajira).
Sehemu ya awali ya vipindi hivyo ni maelezo juu ya namna
uchimbaji mkubwa wa madini unavyoendeshwa kuanzia utafiti wa madini hadi kwenye
uchimbaji wake, miundombinu yakukabiliana na mazingira ilivyowekezwa na
makampuni yanayochimba madini pamoja kiwango cha wafanyakazi wa kitanzania
kwenye sekta hiyo.
Aidha vipindi hivyo vitakua vikieleza pia namna makampuni ya
madini yanavyogeuza vijiji kuwa miji kutokana na uwekezaji wa miundombinu
mbalimbali ikiwemo huduma za umeme na maji kwenye maeneo ya karibu na migodi
hiyo.
Kwenye makala ya mwisho ya vipindi hivyo ambavyo vitaanza
kurushwa kwenye vituo mbalimbali vya televisheni mwishoni mwa mwezi huu
kitaangazia ukuzaji wa ajira kutokana na uchimbaji wa madini ikiwemo maoni ya
wachimbaji wenyewe kwenye migodi husika.
Kahama alisema kwenye sekta hiyo kumekua na Changamoto
nyingi yakiwemo maneno mengi ya upotosha juu ya sekta hiyo na ndio maana
wamekja na vipindi hivyo kutokana na wananchi mbali na kusikia tu lakini pia
watapata kuona kwa picha juu ya hali halisi ilivyo kwenye sekta hiyo.
Changamoto nyingine ni ya hivi karibuni pale waziri wa
nishati na Madini alipoamua kuongeza kiwango cha Tozo kwa wenye migodi bila
kuwashirikisha.
No comments:
Post a Comment