Mkurugenzi
wa Mauzo wa Shirika la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu nchini (AIESEC), Frank
Mushi akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandhi wa habari jijini Dar
es Salaam kuhusu mkutano utakaofanyika Nov.14-18. Kushoto ni Kiongozi
wa maandalizi ya mkutano huo, Gwamaka Mwabuka na Rais wa AIESEC, Echo
Wong
Na Shehe Semtawa
SHIRIKA
la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu nchini (AIESEC), litakuwa mwenyeji wa
mkutano wa vijana zaidi ya 400 kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika
Mashariki utakaozungumzia ushiriki wa vijana katika jumuiya hiyo.
Akizungumza
na wandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo),
jijini Dar es salaam leo, Msemaji wa Shirika hilo, Frank Mushi alisema
mkutano huo utakuwa wa siku tano, kuanzia Novemba 14 hadi 18 mwaka huu.
Alisema mkutano huo unalengo la kuwajengea uwezo wa kujiwezesha katika shughuli mbalimbali za ujasiliamali katika jumuiya hiyo.
Mushi
alisema mkutano huo ni wa sita tangu kuanzishwa shirika hilo miaka 13
iliyopita ambapo zaidi ya wanafunzi 35,000 wamenufaika kwa kujiajiri
katika nyanja mbalimbali za kijasiriamali nchini.
“Katika
mkutano wetu huo tutajadili namana ya kuzuia mchafuko vile vita ya
dunia iliyopita, huko nyma, hivyo kukutana kwetu sisi vijana tutaweza
kujifunza mambo mengi ya msingi na maedeleo katika nchi zetu”alisema
Mushi.
Frank
alizitaja nchi ambazo zitashiriki katika mkutano huo utakaofanyika
jijini Dar es Saam ni pamoja na Kenye, Uganda, Rwanda, Burundi na
wenyeji Tanzania.
No comments:
Post a Comment