Meneja
Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mbando (kushoto) akimkabidhi
Moderm ya Airtel 3.75G Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi
wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo ya Simu ambao ni wadha,mini
wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa inayofanyika mkoani Iringa.
Wengine katika picha ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani na Mwenyekiti wa
Baraza la Usalama Barabarani. Pereira Silima (wapili kulia) na Mkuu wa
Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma. Maadhimisho ya Wiki ya Nenda
kwa Usalama yameanza leo kitaifa Mkoani Iringa.
Waziri
wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, akimkabidhi cheti cha heshima
kwa kuwa wachangiaji katika kampeni ya kupambana na kupunguza ajali
barabarani pamoja na Wiki ya Nenda kwa Usalama kitaifa, Meneja wa
Airtel Kanda za Nyanda za Juu Kusini, Beda Kinunda.Makabidhiano hayo
yalifanyika jana katika ufunguzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa
mkoani Iringa.
Baadhi
ya walemavu wakiingia uwanjani katika uwanja wa Samora mjini Iringa
katika Uzinduzi wa Wiki ya kitaifa ya Nenda kwa Usalama iliyozinduliwa
jana mjini hapa huku Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel ikiwa
mdhamini mkuu.
Mkurugenzi
Mkuu wa Makampuni ya ASAS, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Wiki
ya Nenda kwa Usalama Mkoa wa Iringa, Salim Ahmed, akipokea cheti cha
heshima kwa kuwa wachangiaji katika kampeni ya kupambana na kupunguza
ajali barabarani pamoja na Wiki ya Nenda kwa Usalama kitaifa, kutoka
kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi. Makabidhiano hayo
yalifanyika jana katika ufunguzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa
mkoani Iringa.
Kiongozi
wa Kundi la Wazee Sugu, King Kikii, akiongeza waimbaji wa kundi hilo
kutoa burudani ya muziki katika uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya
Nenda kwa Usalama Kitaifa iliyoanza jana mkoani Iringa.
No comments:
Post a Comment