Kikosi cha kwanza cha Yanga kilichocheza na kushinda mabao 4-1
dhidi ya JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa. Kikosi hichi kinajumuisha
wakali wote wa kigeni waliosajiliwa Yanga msimu huu; Yaw Berko (kulia
waliosimama), Didier Kavumbagu (katikati nyuma), Mbuyu Twite (kulia
waliochuchumaa), akifuatiwa na Hamis Kiiza na Haruna Niyonzima (wa pili
kushoto waliochuchumaa).
SHIRIKISHO la Soka nchini (TFF), limesema ni ruksa kwa klabu
yoyote kuwachezesha kwa pamoja wachezaji wote wakigeni waliosajiriwa na klabu katika
Ligi Kuu ya Vodacom Tazania Bara.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Ofisa Habari wa TFF Boniface
Wambura alisema kuwa, sheria na kanuni za Ligi Kuu zinaruhusu klabu moja
kusajili wachezaji wa kigeni watano, ambapo hakuna kiwango cha kuwatumia kwa
pamoja katika mechi ya ligi hiyo.
Wambura amelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya kuwepo kwa uvumi
kwamba Mabingwa wa Kombe la Kagame Yanga ya jijini Dar es Salaam, inaweza
kupokonywa ponti tatu ilizozipata katika mchezo wa juzi dhidi ya JKT Ruvu, baada
ya kuwachezesha wachezaji wake wote wa kigeni.
Katika mechi hiyo, Yanga iliwapanga kikosi chwa kwanza wakali wake Mghana Yaw Berko, Didier Kavumbagu wa Burundi, Haruna Niyonzima na Mbuyu Twite wa Rwanda na Mganda Hamis Kiiza, kabla ya leo asubuhi kuibuka kwa tetesi kuwa Wanajangwani hao watapoteza pointi kwa kuwapanga wote.
Katika mechi hiyo, Yanga iliwapanga kikosi chwa kwanza wakali wake Mghana Yaw Berko, Didier Kavumbagu wa Burundi, Haruna Niyonzima na Mbuyu Twite wa Rwanda na Mganda Hamis Kiiza, kabla ya leo asubuhi kuibuka kwa tetesi kuwa Wanajangwani hao watapoteza pointi kwa kuwapanga wote.
“Huo ni uvumi tu, Yanga hawawezi kunyanganywa point zao kwa kuwa
hakuna utata wowote wa kuwachezesha wachezaji wa kigeni wote waliosajiliwa ili
waisaidie timu kulingana na sheria za
Ligi Kuu,” alisema Wambura.
Wambura alisema kuwa TFF wanakusudia kupunguza idadi ya wachezaji
wa kigeni katika Ligi Kuu msimu wa mwaka 2013/14 kutoka wachezaji watano hadi
kufikia watatu na si mwaka huu.
No comments:
Post a Comment