Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, September 30, 2012

KINONDONI ,ILALA WATINGA FAINALI MASHINDANO YA POOL TAIFA


Baadhi ya Wachezaji waliofanikiwa kutinga nusu fainali 
Mchezaji wa Singles wanaume kutoka Klabu ya Blue Hose ya Mbeya, Solomon Elias akicheza ambye ni mlemavu wa kuongea(BUBU) kafikia hatua ya fainali
Na Mwandishi wetu,Mwanza
MKURUGENZI  wa michezo  katika Wizara ya Habari, Utamaduni , Vijana na Michezo, Leonard Thadeo leo anatarajia kuwa mgeni rasmi katika kilele cha fainali za taifa za mashindano ya mchezo wa pool ya 'Safari Lager National Pool Championship 2012'.
Fainali hizo za mashindano hayo yanayodhaminiwa na wadhamini wakuu wa mchezo wa pool nchini, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager zinafanyikia kwenye ukumbi wa hoteli ya Monarch iliyopo mkoani hapo.
Mchezo wa fainali kwa upande wa timu utazikutanisha timu za Meeda ya Kinondoni na Kayumba ya Ilala zote kutoka Dar es salaam.
Meeda ilifanikiwa kutinga hatua ya fainali baada ya kuichapa Anatory ya Morogoro magoli 13-10 kwenye hatua ya nusu fainali, huku Kayumba ikitinga hatua hiyo baada ya kuichapa 2eyes ya Arusha magoli 13-9 katika mchezo wa nusu fainali.
Kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanaume), Solomoni Elias kutoka mkoa wa Mbeya alikuwa wa kwanza kutinga fainali baada ya kumfunga Ally Nada wa Manyara magoli 4-0 katika hatua ya nusu fainali na hivyo kumsubiri mshindi kati ya Fayuu Staniley wa Arusha na Athuman Seleman Morogoro kwa  ajili ya kucheza  fainali.
Na katika upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanawake), Cesilia KIleo wa Kilimanjaro na Betty Sanga wa Mbeya watachuana vikali katika hatua ya fainali baada ya kushinda michezo yao ya nusu fainali.
Wakati Cecilia Kilio alimchapa Sada Tulla wa Shinyanga magoli 4-3, Betty Sanga yeye alitinga fainali baada ya kumgalagaza vibaya  Anna Peter wa Iringa magoli 4-0.
Bingwa kwa upande wa timu ataondoka na fedha taslim Sh.Mil.5, kombe  na medali za dhahabu kwa wachezaji wa timu nzima, wakati ambapo bingwa kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanaume) atajizolea Sh.500,000 na bingwa wa mchezaji mmoja mmoja (wanawake) atazawadiwa Sh.350,000.
Mbali ya zawadi kwa washindi hao lakini kuanzia mshindi wa pili kwa upande wa timu hadi wa mwisho kila moja itaondoka na zawadi za fedha taslim kulingana na nafasi lakini pia zawadi hizo ni kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja wanaume na wanawake.
 Wachezaji wa Klabu ya Meeda ya jijini Dar es Salaam wakiwa na Mkurugenzi wao mara baada ya kutinga fainali
 Watu wakifuatilia mchezo wa pool
 Wakifuatilia
 Wakifuatilia
 Wachezaji wakishindana kulagi
 Wakifuatilia
 Kocha wa timu ya Taifa ya Pool, akifurahi na baaadhi ya wachezaji
 Mkurugenzi wa Meeda akifurahi na kijana wake mara baada ya kupata A
 Mwana Dada kutoka Mbeya akicheza a,baye katinga fainali pia

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...