huu ndio mlango wa kuingia ndani ya mjengo wenyewe, Madam Ritta anaingia hapa....
SHINDANO la kusaka
vipaji vya uimbaji la Bongo Star Search limeanza tena, ambapo mwaka huu itakuwa
na washiriki 12 na mmoja wao atakayeshinda ataibuka na kitita cha Shilingi
MIlioni 50.
Kila mwaka shindano
hili ninazidi kuboreshwa na kuwa na muonekano bora, safari hii shindano hilo
linafahamika kama Epiq Bongo Star Search (EBSS) kutokana na kampuni ya Simu ya
Zantel kuamua kuunga mkono kwa kutoa ufadhili.
Kwenye maboresho ya
EBSS washiriki wote 12 watakuwa wakiishi katika nyumba moja, wakiwa ndani
watafanya kazi mbalimbali pamoja na kupata mafunzo ya muziki kutoka kwa
wakufunzi wenye utaalamu wa masuala ya muziki.
Jaji Mkuu wa EBSS
Ritta Paulsen maarufu kama `Madame Ritta'alisema jumba hilo lenye kila kitu
ndani ni moja ya alama kuu ya maboresho ya shindano hilo na kuwa la Kimataifa
zaidi.
"Jumba la EBSS
ni moja ya nyumba yenye ubora nchini, washiriki wataishi humo kwa muda wa wiki
nane wakati kusaka msindi wetu, wakiwa ndani watafurahi, watajifunza mambo
mbalimbali pamoja na kuongeza uzoefu wa kuishi kwa kujituma," alisema
Ritta.
Ufunguzi wa jumba
hilo ulifanyika mapema wiki hii, ambapo watu mbalimbali wakio\wemo viongozi wa
Zantel walishuhudia sherehe ya uzinduzi.
ENEO ILIPO EBSS HOUSE
Jumba hilo la
kifahari lipo katika eneo la Kawe
Mzimuni, imezungukwa na majumba ya kifahari pamoja na kambi ya Jeshi ya Lugalo.
Sehemu hiyo ni
tulivu, kitu ambacho kinasababisha washiriki kujifunza vizuri wakiwemo ndani ya
nyumba pamoja na kufanya shughuli zao kwa utulivu mkubwa.
NDANI YA NYUMBA.
Ukumbi wa mazoezi:
Mara unapoingia ndani kupitia lango kuu wenye kunakshiwa na marembo ya
Kizanzibar, utakumbana na chumba kikubwa, ambapo hapo ndipo sehemu maalum ya
kufanyia mazoezi ya uimbaji.
Kwenye chumba hicho
kuna vyombo mbalimbali vya muziki vitakavyotumiwa na washiriki wakati mazoezi
yao ya vitendo.
Dadasa: Kwa upande wa
kushoto ndani ya jumba hilo kuna chumba kidogo chenye viti pamoja na ubao. Kwa
mujibu wa Muandaaji wa Shindano hilo Ritta paulsen chumba hicho kitatumika kama
darasa, washiriki watapewa mafunzo mbalimbali ya jinsi ya kutumia toni za
muziki kwa nadharia.
Jiko: Upande wa mbele
kabisa kuna chumba maalum kwa ajili ya kupikia, humo kuna vifaa vyote vya
mazuala ya upishi, hivyo itakuwa rahisi kwa washiriki wenyewe kupika chakula
wanachotaka endapo hawatapenda kula vile wanavyopikiwa na wapishi maalum
waliokuwemo ndani ya nyumba.
Vyumba vya kulala
washiriki: Katika shindano hilo kunakuwa na mtu ambaye anaitwa Mkuu wa nyumba,
huyu ni mshiriki ambaye ameshinda kutokana na kufanya jitiahada kubwa katika
kazi zake na hukabidhiwa kazi ya kuwaongoza wenzake. Safari hii Mkuu wa nyumba
atakuwa na chumba chake cha kulala chenye kila kitu ndani yake, hivyo anaweza
kujifanyia shughuli zake hata akiwa ndani ya chumba chake. Kwa upande wa
washiriki kuna chumba kikubwa chenye vitanda vitakavyowatosheleza kulala
washiriki wote.
Vitu Vingine: Baadhi
ya vitu vingine vilivyokuwemo kwenye nyumba hiyo ni pamoja na bwawa la
kuogelea, chumba cha kulia chakula, sehemu ya kupumzikia pamoja na bustani
nzuri ya kufanyia mazongezi.
Washiriki
waliofanikiwa kuingia ndani ya nyumba hiyo ni Godfrey Kato, Husna Nassoro,
Linias Mhaya, Menynah Atiki, Norman Severina, Nsami Nkwabi, Nshoma
Ng'hangasamala, Salma Mahin, Vicent Mushi, Wababa Mtuka na walter Chilambo.
No comments:
Post a Comment