MANCHESTER, England
Wakati
Man United ikihaha kujaribu kuipenya safu ya ulinzi ya Wigan, huku
Chicharito akikosa penati ya kipindi cha kwanza, aina sahihi ya
upiganaji wa Scholes ukairejesha mchezoni United kipindi cha pili
KOCHA wa Manchester United ya England, Sir
Alex Ferguson amempigia saluti kiungo wake Paul Scholes, baada ya
mkongwe huyo kucheza mechi ya 700 akiwa na Mashetani Wekundu, huku
akifunga bao moja katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Wigan huko Old
Trafford.
Wakati United ikihaha kujaribu kuipenya
safu ya ulinzi ya Wigan, huku Javier Hernandez ‘Chicharito’ akikosa
penati ya kipindi cha kwanza jana Jumamosi, aina sahihi ya upiganaji wa
Scholes ukairejesha mchezoni United kipindi cha pili alichotikisa nyavu.
Nyota huyo mwenye miaka 37, alifunga bao
hilo akimlazimisha mlinda mlango wa Wingani Ali Al-Habsi kufanya jaribio
la pili la kuokoa hatari baada ya kupangua krosi ya winga Nani.
Baada ya bao hilo United ikasimama imara na kufunga mengine kupitia Chicharito, Alexander Buttner na Nick Powell.
Bao la Scholes limemfanya apanue rekodi ya
utikisaji nyavu katika mechi hiyo ya kihistoria kwake na kuthibitisha
kile United chini ya Ferguson ilichokosa kutoka kwa nyota huyo,
aliyeshawishiwa kurudi dimbani Januari mwaka huu kuokoa jahazi baada ya
kuwa alishastaafu.
"Ndicho kitu ambacho sisi daima tulikuwa
tukikimbuka kuhusu Paul, namna anavyofanya maajau kama hayo afikapo eneo
la hatari la wapinzani," alisema Ferguson baada ya kumalizika kwa mechi
hiyo.
"Ni wazi kwamba ameshakuwa mkubwa kiumri,
yeye hajaweza kufanya haya. Kwamba yeye ahitaji kufanya hivyo kwa sababu
sisi tunapenda kumtumia kama kiungo wa kati, sio wa mbele katika
ufungaji mabao.
"Lakini ndicho alichofanya dimbani,
alifunga bao katika mechi yake ya 100, akafanya hivyo katiika mechi ya
300, akarudia tena wakati akicheza mechi ya 400, 500 na sasa amerejea
hilo katika mechi ya 700. Ni jambo la kushangaza sana," alisema Fergie
aliyemrejesha dimbani.
No comments:
Post a Comment