Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, September 22, 2012

MABINGWA WA UGANDA NA TANZANIA KUPAMBANA OCTOBER 14


THOMAS MASHALI TANZANIA
huyu ndiye med sebyala kutoka uganda-2012 atapambana na mbondia mtukutu THOMAS MASHALI  katika ukumbi wa friends corner ulioko manzese jijini dar-es-salaam ,kuwania ubingwa wa afrika mashariki na kati ktk uzito wa  kati [middle ] kg 72.5.
 
 
MED SEBYALA ni bingwa wa uganda katika uzito huo wakato thomas mashali ni bingwa wa tanzania wa TPBO uzito huo huo wa kati.
 
 
med sebyala
pambano hili linawakutanisha mabondia wakali na wakatili wawapo ulingoni kwa kanda hii ya afrika mashariki .
 
 
wakati med sebyala ameshawahi kupambana na francis cheka mjini morogoro kuwania ubingwa wa UBO ,Na pia akapambana na bondia mkongwe nchin RASHID MATUMLA jijini dar-es-salaam na kutowa upinzania mkali kiasi cha kumaliza mapambano yote hayo kwa kushindwa hwa points ,mpinzania wake THOMAS MASHALI yeye amekuwa akiwapa adhabu kali wapinzani wake kwa kuwatwanga kwa knock-out za mapema tu isipokuwa SELEMAN GALILE pekee aliyefanikiwa kunaliza pambano la kugombea ubingwa wa TPBO uzito wa kati.
 
 
TPBO inawataka wapenzi wa ngumi za kulipwa wa jiji la dar-es-salaam na vitongoji vyake kukaa tayari na kujiandaa vyema kwa kushuhugia mpambano wa mabingwa wa nchi zao wakimenyana siku hiyo .
 
 
pambano hili ni mahususi kwa ajili ya kumkumbuka baba wa faifa hayati mwl julius kamarage nyerere.
 
tumeamuwa kuwa kila tarehe ya kumbukumbu  ya kifo cha mwalimu nyerere TPBO itakuwa inaandaa mapambano ya ngumi ,ikiwa ni hrshima kubwa kwa utawala wake wa serikali ya awamu ya kwanza kwa jinsi alivyokuwa akisaidia michezo yote bila kubaguwa , kinyume na sasa hivi ambapo mchezo wa ngumi za aina zote umetupwa , na hauthaminiwi ,na hata wdhamini wanauona kama ni mchezo wa wahalifutunasikitika sana tuonapo kuna jamii ya watanzania wenzetu wanathaminiwa michezo yao ,wakati watanzania wengine wanadharauliwa na kubaguliwa katika mochezo.
 
 
EEEEH MWENYEZI MUNGU MLAZE PEMA PAPONI HAYATI MWL JUIIUS KAMBARAGE NYERERE ,NA UWALAANI WOTE  WALETAO UBAGUZI MICHEZONI
 
                  AMEEN

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...