Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou akimkaribisha Mgeni
rasmi katika maadhimisho ya siku ya Amani Duniani aliyekuwa Naibu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Asha-Rose Migiro.
Dkt. Asha-Rose Migiro akisalimiana na Balozi wa Nigeria nchini Tanzania Dr. Ishaya Nanjabu.
Dkt. Migiro akiteta jambo na Dkt. Kacou wakati Balozi wa Nigeria Dr.
Nanjabu akizungumza na mmoja wa maafisa wa jeshi hapa nchini wakati
wakisubiri maandamano ya Amani.
Dkt. Migiro sambamba na Dkt. Kacou wakielekea kupokea maandamano ya
Wanafunzi wa Shule mbalimbali jijini Dar katika maadhimisho ya siku ya
Amani Duniani.
Mgeni rasmi Dkt. Migiro (katikati), Dkt. Kacou pamoja na Balozi wa
Nigeria nchini Dr. Nanjabu (kushoto) wakiwa wamebeba sanamu mfano wa
ndege aina ya Njiwa ikiwa ni Ishara ya Amani.
Mgeni rasmi Dkt. Asha-Rose Migiro akiimba nyimbo za kuhamasisha Amani pamoja na washiriki wa maandamano ya siku Amani Duniani.
Afisa
Habari kutoka kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa Stella Vuzo
akitoa utambulisho wa meza kuu.Katikati ni Mgeni rasmi Aliyekuwa Naibu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Asha-Rose Migiro, Mratibu Mkazi wa
Umoja wa Mataifa Dkt. Alberic Kacou (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa
shirika lisilo la kiserikali la Right to Play Bw. Francis Rwiza (kulia),
Balozi wa Nigeria nchini Tanzania Dr. Ishaya Nanjabu na Wa pili kulia
ni Program Manager wa Global Network of Religions for Children (GNRC)
Bi. Elizabeth Mwase.
Wanafunzi wa shule mbalimbali za jijini Dar wakati wa maadhimisho ya
Siku ya Amani Duniani yenye Kauli mbiu "AMANI ENDELEVU KWA UENDELEVU WA
MASIHA YA BAADAE".
Mmoja
wa viongozi wa madhehebu ya Dini kutoka BAKWATA akitoa sala wakati w
ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya Amani Duniani leo jijini Dar es
Salaam.
Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa hapa nchini Dkt. Alberic Kacou akitoa hotuba
wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Amani Duniani ambapo
amerejea kusisitiza kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban
Ki-Moon katika ujumbe wake wa amani mwaka huu.
Amesema
katika Siku ya Kimataifa ya Amani, Umoja wa Mataifa unatoa wito wa
kusitishwa kabisa kwa mapigano mahali mbalimbali duniani kwa kuwa
mapigano ya silaha yanashambulia mihimili muhimu ya maendeleo endelev
Bw.
Kacou pia ametumia fursa hiyo kulipongeza Bunge la Tanzania kwa dhima
yake ya kuhamasisha Utawala Bora na kupiga vita ufisadi ili kuleta
maendeleo ya taifa.
Mgeni
rasmi katika maadhimisho ya siku ya Amani Duniani aliyekuwa Naibu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Asha-Rose Migiro akizungumza wakati
wa maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani leo jijini Dar es Salaam,
ambapo pamoja na mambo mengine amesema Tanzania itaendelea kuwa mfano wa
jinsi demokrasi inavyofanya kazi katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Aidha
amesema mchakato unaoendelea wa mabadiliko ya katiba umewaweka wanaume
na wanawake wa Tanzania katika nafasi ya kuamua kuhusu kuimarisha
manufaa ya Kidemokrasia, kuimarisha utawala bora na haki za binadamu.
Pichani
ni baadhi ya mabalozi wanaowakilisha nchi zao pamoja na maafisa wa
mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini wakisiliza hotuba ya mgeni rasmi
Dkt. Asha-Rose Migiro (hayupo pichani).
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwamo wawakilishi kutoka Serikalini,
Mabalozi na Viongozi kutoka Ofisi za Kibalozi na Wanafunzi kutoka shule
mbalimbali za jijini Dar.
Mwanafunzi wa shule ya msingi Airwing Brenda Simon aliyeshiriki shindano la Insha ya Siku ya Amani Duniani.
Mshindi
wa Insha wa maadhimisho ya siku ya Amani Duniani kutoka Shule ya
Sekondari Kibasila akisoma Insha yake mbele ya wageni waalikwa hawapo
pichani.
Mkurugenzi
wa shirika lisilo la Kiserikali la Right to Play Bw. Francis Rwiza
akimkabidhi cheti pamoja na zawadi mshindi wa Insha ya maadhimisho ya
siku ya Amani Duniani mwanafunzi wa shule ya msingi Airwing Brenda
Simon.
Wanafunzi kutoka shule ya msingi Buguruni Viziwi wakitoa burudani wakati wa sherehe za maadhimisho hayo.
Dkt. Asha R0se Migiro akiimba pamoja na wanafunzi wa shule mbalimbali za jijini Dar wakati akiondoka ukumbini hapo.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa hapa nchini Dkt.Alberic Kacou
akimsindikiza mgeni rasmi Dkt. Asha-Rose Migiro baada ya shereh za
maadhimisho hayo.
Dkt. Asha-Rose Migiro akifanyiwa mahojiano na vyombo vya habari nchini.
Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania Dkt. Alberic Kacou akiteta jambo na
baadhi ya mabalozi waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya Amani
Duniani zilizofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Afisa
Habari kutoka kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa Stella Vuzo (wa
nne kushoto) pamoja na wadau wakifurahia sherehe za maadhimisho ya siku
ya Amani Duniani.
Na.Mwandishi wetu
Aliyekuwa
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Asha Rose Migiro amesema ili
amani idumu nchini kuna ulazima wa raslimali za nchi zitumika kwa
maendeleo.
Migiro amesema amani iliyopo nchini ni ya kujivunia na inahitaji kutunzwa na kuheshimiwa.
Amesema hayo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Amani duniani iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Dkt.
Migiro amesema ili amani idumu ni lazima iwepo mipango madhubuti ya
kuhakikisha uchumi unakua kwa kila nchi na kuhakikisha kwamba raslimali
za nchi zinatumika vizuri ili kuleta maendeleo.
Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na mabalozi na baadhi ya viongozi wa serikali na wabunge.
No comments:
Post a Comment