Na
Elizabeth John
MUIGIZAJI
wa filamu nchini, Mohamed Nurdin ‘Chekibudi’ ameonekana kupanda kwa kasi katika
soko la sanaa, baada ya kuachia filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la
‘Dikteta’, ambayo imeanza kufanya vizuri sokoni.
Filamu
hiyo mpya inayoonesha ukandamizaji wa familia, imekamilika na kuingizwa sokoni
hivi karibuni, ambapo tayari imeanza kufanya vizuri katika mauzo, hasa
katika baadhi ya maeneo ya jijini Dar es Salaam, ikisambazwa na kampuni ya
Steps Entertaiment.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana, Chekibudi alisema, filamu hiyo ameiandaa ili
kuonesha ukandamizaji uliopo ndani ya baadhi ya familia katika maisha ya kila
siku, na amefarijika kuona Watanzaania wakiipokea vema sokoni.
Alisema
baada ya kuangalia hilo, aliamua kuweka wazo lake katika
filamu ili kuwafikishia ujumbe watu wengi zaidi na ikawa kama
ni moja ya kazi za wasanii kuelimisha na kufundisha jamii.
“Unajua
unapokuwa msanii unatakiwa kuwa mbunifu katika mambo mengi na ndiyo maana kila
kukicha tunaangalia ni jinsi gani tutawakumbusha wenzetu matatizo ambayo
yanaepukika,” alisema Chekibudi.
Chekibudi
alishawahi kufanya vizuri alipokuwa katika kundi la sanaa la ‘Splendid’, na
katika filamu hiyo ya ‘Dikteta’ amewashirikisha nyota wengine kama, Cojack,
Philipo, Munira Sultan, Snura Mush, Coletha Reymond pamoja na nyota wengine.
No comments:
Post a Comment