DAR ES SALAAM, Tanzania
MWANDISHI wa habari wa Kampuni ya Free Media Ltd
inayochapisha magazeti ya Tanzania Daima na Sayari, Agnes Yamo, amefariki dunia
alfajiri ya leo kwenye Hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Habari Mseto, Mhariri Mtendaji wa Tanzania
Daima, Absalom Kibanda, amesema familia ya marehemu Agnes imethibitisha kutokea
kwa msiba huo na kuwa marehemu amekufa wakati akipata matibabu kutokana na upungufu
wa damu.
Kibanda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri
nchini (TEF), aliongeza kuwa msiba wa Agnes uko nyumbani kwa kaka yake Buguruni
Sokoni (Rozana) kwenye mafleti ya Muhimbili.
Enzi za uhai wake, Agnes aliyezaliwa Agosti 9, 1978, alikuwa
mwandishi aliyefanya kazi Kampuni ya Habari Corporation, kabla ya
Tanzania Daima alikofanya uandishi kwa muda na baadaye kugeukia Idara ya
Matangazo ya Free Media Ltd inayochapisha gazeti hilo,
hadi umauti ulipomkuta.
Kwa mujibu wa Kibanda, mipango ya mazishi inaendelea
kufanyika nyumbani kwa kaka wa marehemu, ambapo mwili unatarajiwa kusafirishwa
kesho Jumatano jioni kwenda Morogoro yatakakofanyika maziko yake.
Shughuli za kutoa heshima za mwisho na kuuaga mwili wa
marehemu zinatarajiwa kufanyika nyumbani hapo kwa kaka yake Buguruni, kabla ya
kusafirishwa. Mungu ailaze ROHO ya marehemu mahali pema PEPONI. Ameeeeeen
No comments:
Post a Comment