Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, September 22, 2012

YANGA YAIBOMOA JKT RUVU MABAO 4-1



Wachezaji Hamis Kiiza wa Yanga (kushoto), akiwania mpira na Ally Khan wa JKT Ruvu wakati timu hizo zilipopambana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo. 
 Yanga ikiwa na kocha wake msaidizi fred minziro

imefanikiwa kupata ushindi wa mabao 4-1 mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa taifa dar es salaam.
Katika dakika kumi za mwisho wapenzi wa yanga walijikuta wakiomba mchezo umalizike baada ya jkt ruvu kucheza mchezo mkali. Wapenzi wa simba walionekana kushangilia hali hiyo ambayo hata hivyo matokeo yakawa 4-1.

Katika mchezo wa chamazi azam imeibuka na ushindi wa bao 1-0. Bao la azam limepatikana dakika ya 26 ya mchezo kupitia kwa kipre tchetche.
Cledo mwaipopo ameipatia jkt ruvu bao moja baada ya kazi nzuri ya omar changa na sospeter manyasi.
  Yanga imepata bao la nne kupitia kwa didier kavumbangu baada ya kipa jkt ruvu kuutema mpira.
 dakika ya 52 simon msuva aliipatia yanga bao la tatu baada ya kuambaa ambaaa na mpira na kupachika wavuni. mapumziko yanga imetoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 2-0.

 Bao la kwanza limepatikana dakika ya 4 ya mchezo kupitia kwa nadir haroub canavaro' baada ya kazi nzuri ya haruna niyonzima na athuman idd chuji
Dakika 31 yanga ilipata bao la pili kupitia kwa

didier kavumbagu akimalizia chuji. Katika kipindi cha kwanza yanga iliweza kutawala mchezo kwa kufanya mashambulizi mengi katika lango la jkt ruvu.

 Kwa upande wa jkt ikitumia wachezaji wake sospeter manyasi na omar changa walishindwa kufanya makeke makali hivyo mipira mingi kutoka nje.

  Kesho kuna mechi tatu ambapo mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara msimu uliopita simba itavaana na Ruvu shootingStars mchezo utakaofanyika kwenye uwanja wa taifa dar es salaam. 
Mchezo mwingine utafanyika kwenye uwanja wa chamazi utazikutanisha african lyon dhidi ya tanzania prisons na mechi nyingine itakukuwa kwenye uwanja mkwakwani mkoani tanga mgambo jkt ikiwakaribisha. Kagera sugar. Kilatimu inahitaji pointi tatu ili iweze kukaa sawa katika msimamo wa ligi kuu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...